Kimara (Australia)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kimara (pia Kimarra) ni lugha ya Kigunwinyguan nchini Australia inayozungumzwa na Wamara katika jimbo la Northern Territory. Isichanganywe na lugha ya Kimara inayozungumzwa nchini Uhindi.

Katika sensa ya mwaka 2006, idadi ya wasemaji wa Kimara ilihesabiwa kuwa watu 58 tu, yaani lugha iko hatarini mwa kutoweka kabisa hivi karibuni. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kimara kiko katika kundi la Kimarran, yaani inahusiana na Kialawa na Kiwandarang.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kimara (Australia) kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.