Kilomita ya ujazo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kilomita ya ujazo (kifupi km³) ni kipimo cha mjao chenye urefu, upana na kimo cha kilomita moja. Ni kiwango katika vipimo sanifu vya kimataifa.

Kilomita moja ya ujazo inalingana na bilioni moja mita za ujazo.

1 km³ = 109 m³ = 1 000 000 000 m³

Kwa mfano mjao wa bahari hutajwa kwa kipimo hiki. Bahari zote za dunia huhesabiwa kuwa na kiasi cha 1,385,990,800 km³ za maji.