Nenda kwa yaliyomo

Kikohozi kikuu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kikohozi kikuu
Mwainisho na taarifa za nje
Kundi MaalumuInfectious diseases Edit this on Wikidata
ICD-10A37.
ICD-9033
DiseasesDB1523
MedlinePlus001561
eMedicineemerg/394 ped/1778
MeSHD014917

Kikohozi kikuu, au kikohozi cha siku 100, ni ugonjwa unaosababishwa na bakteria.[1][2] Mwanzoni, dalili huwa sawa na za mafua ya kawaida ambapo mtu huwa na mafua, homa na kikohozi cha kiwango kidogo. Dalili hizi kisha hufuatiwa na vipindi vya kikohozi kikali kwa wiki kadhaa. Sauti kali ya “whoop” inaweza kutoka kufuatia tukio la kukohoa mtu anapovuta pumzi.[2] Kikohozi hiki kinaweza kudumu kwa zaidi ya siku mia moja au wiki kumi.[3] Mtu anaweza kukohoa sana hadi akatapika, akavunjika mbavu, au akawa mchovu sana kutokana na juhudi za kukohoa.[2][4] Watoto wa chini ya mwaka mmoja wanaweza kuwa na kikohozi kidogo au hata wasiwe nacho na badala yake wawe na vipindi ambapo hawapumui.[2] Kipindi cha kati ya kuambukizwa na kuanza kwa dalili kwa kawaida huwa siku saba na kumi.[5] Ugonjwa huu unaweza kutokea kwa watu waliochanjwa, lakini kwa kawaida dalili huwa hafifu.[2]

Kisababishi na utambuzi

[hariri | hariri chanzo]

Kifaduro husababishwa na bakteria ya Bordetella pertussis. Kifaduro ugonjwa unaosambazwa hewani unaoenea haraka kwa kikohozi na chafya ya mtu aliyeambukizwa.[6] Watu wanaweza kuwaambukiza wengine kutoka mwanzo wa dalili hadi takriban wiki tatu baada ya kuanza kwa matukio ya kukohoa. Watu wanaotibiwa kwa antibiotiki huwa hawaambukizi wengine baada ya siku tano.[7] Utambuzi hufanywa kwa kuchukua sampuli kutoka kwa sehemu ya nyuma ya pua na koo. Sampuli hii kisha inaweza kuchunguzwa kwa kukuza vimelea au kwa kukuza akala ya DNA.[8]

Kinga na matibabu

[hariri | hariri chanzo]

Kinga huwa hasa kwa chanjo ya dawa ya chanjo.[9] Chanjo ya kwanza hupendekezwa kati ya wiki sita na nane baada ya kuzaliwa huku vipimo vinne vya dawa vikipeanwa katika miaka miwili ya kwanza baada ya kuzaliwa.[10] Chanjo hii huisha nguvu baada ya muda, hivyo vipimo zaidi hupendekezwa kwa watoto wakubwa na watu wazima.[11] Antibiotiki zinaweza kutumika kuzuia ugonjwa huu katika watu walio katika hatari kubwa ya kuambukizwa ugonjwa huu.[12] Kwa watu walioambukizwa, antibiotiki hufaa ikiwa watazitumia wiki tatu baada ya dalili za kwanza, la sivyo hazina manufaa mengi kwa watu wengi. Katika watoto wa chini ya mwaka mmoja na kina mama wajawazito, antibiotiki hupendekezwa wiki sita baada ya kuanza kwa maambukizi. Antibiotiki zinazotumika hujumuisha erythromycin, azithromycin, au trimethoprim/sulfamethoxazole.[7] Hakuna ushahidi wa kutosha kuhusu manufaa ya matibabu kwa kikohozi hiki.[13] Idadi kubwa ya watoto wa chini ya mwaka mmoja huhitajii kulazwa hospitalini.[2]

Epidemiolojia na historia

[hariri | hariri chanzo]

Inakadiriwa kwamba kifaduro huwaathiri watu milioni 16  kote duniani kila mwaka.[13] Idadi kubwa ya visa hutokea katika mataifa yanayostawi na watu wa umri wowote wanaweza kuathiriwa[9][13] Mwaka wa 2013, ugonjwa huu ulisababisha vifo 61,000 – vilivyoshuka kutoka vifo 138,000 mwaka wa 1990.[14] Karibu 2% ya watoto wanaoambukizwa wakiwa wa chini ya mwaka mmoja hufa.[4] Maelezo ya mizuko ya ugonjwa huu yalitolewa kwa mara ya kwanza katika karne ya 16. Bakteria inayosababisha ugonjwa huu ilitambuliwa mwaka wa 1906. Chanjo yake ilipatikana katika miaka ya 1940.[5]

  1. Carbonetti NH (Juni 2007). "Immunomodulation in the pathogenesis of Bordetella pertussis infection and disease". Curr Opin Pharmacol. 7 (3): 272–8. doi:10.1016/j.coph.2006.12.004. PMID 17418639.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. 2.0 2.1 2.2 2.3 2.4 2.5 "Pertussis (Whooping Cough) Signs & Symptoms". Mei 22, 2014. Iliwekwa mnamo 12 Februari 2015.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. "Pertussis (Whooping Cough) Fast Facts". cdc.gov. Februari 13, 2014. Iliwekwa mnamo 12 Februari 2015.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. 4.0 4.1 "Pertussis (Whooping Cough) Complications". cdc.gov. Agosti 28, 2013. Iliwekwa mnamo 12 Februari 2015.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  5. 5.0 5.1 Atkinson, William (Mei 2012). Pertussis Epidemiology and Prevention of Vaccine-Preventable Diseases (tol. la 12). Public Health Foundation. ku. 215–230. ISBN 9780983263135.{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  6. "Pertussis (Whooping Cough) Causes & Transmission". cdc.gov. Septemba 4, 2014. Iliwekwa mnamo 12 Februari 2015.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  7. 7.0 7.1 "Pertussis (Whooping Cough) Treatment". cdc.gov. Agosti 28, 2013. Iliwekwa mnamo 13 Februari 2015.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  8. "Pertussis (Whooping Cough) Specimen Collection". cdc.gov. Agosti 28, 2013. Iliwekwa mnamo 13 Februari 2015.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  9. 9.0 9.1 Heininger U (Februari 2010). "Update on pertussis in children". Expert review of anti-infective therapy. 8 (2): 163–73. doi:10.1586/eri.09.124. PMID 20109046.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  10. "Revised guidance on the choice of pertussis vaccines: July 2014" (PDF). Wkly Epidemiol Rec. 89 (30): 337–40. Julai 2014. PMID 25072068.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  11. "Pertussis vaccines: WHO position paper". Wkly Epidemiol Rec. 85 (40): 385–400. Okt 1, 2010. PMID 20939150.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  12. "Pertussis (Whooping Cough) Prevention". cdc.gov. Oktoba 10, 2014. Iliwekwa mnamo 13 Februari 2015.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  13. 13.0 13.1 13.2 Wang, K; Bettiol, S; Thompson, MJ; Roberts, NW; Perera, R; Heneghan, CJ; Harnden, A (22 Septemba 2014). "Symptomatic treatment of the cough in whooping cough". The Cochrane database of systematic reviews. 9: CD003257. doi:10.1002/14651858.CD003257.pub5. PMID 25243777.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  14. GBD 2013 Mortality and Causes of Death, Collaborators (17 Desemba 2014). "Global, regional, and national age-sex specific all-cause and cause-specific mortality for 240 causes of death, 1990-2013: a systematic analysis for the Global Burden of Disease Study 2013". Lancet. 385 (9963): 117–71. doi:10.1016/S0140-6736(14)61682-2. PMID 25530442. {{cite journal}}: |first1= has generic name (help)CS1 maint: date auto-translated (link) CS1 maint: numeric names: authors list (link)