Kihadza

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kihadza (au Kitindiga) ni lugha ya nchini Tanzania inayozungumzwa na Wahadza (Watindiga). Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kihadza hailingani na lugha yoyote nyingine. Ingawa ina fonimu za pekee kama zile za Kisandawe, si mojawapo ya lugha za Kikhoisan.

Mwaka wa 2000 idadi ya wasemaji wa Kihadza imehesabiwa kuwa watu 1,000 tu. Hata hivyo watoto bado wanaendelea kujifunza lugha ya wazazi wao, kwa hiyo haionekani kama lugha ambayo itatoweka hivi karibuni.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kihadza kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.