Khalilou Fadiga

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
{{{jinalamchezaji}}}
Maelezo binafsi
Tarehe ya kuzaliwa {{{tareheyakuzaliwa}}}
Mahala pa kuzaliwa    {{{nchialiozaliwa}}}

* Magoli alioshinda

Khalilou Fadiga (amezaliwa 30 Desemba 1974) alikuwa mwanakandanda wa Senegal na Ubelgiji ambaye mwisho alicheza katika kiungo cha kati kwa klabu ya Germinal Beerschot Antwerpen ya Ubelgiji.

Wasifu wa Klabu[hariri | hariri chanzo]

Wasifu wa Mapema[hariri | hariri chanzo]

Fadiga alihamia nchi ya Ufaransa alipokuwa na umri wa miaka sita. Fadiga alianza wasifu wake katika klabu ya Paris Saint-Germain ya Ufaransa, lakini alishindwa kufurahisha hisia za meneja, na hivyo basi alihamishiwa katika klabu mwenzao ya Paris, Red Star 93, kabla ya kuhamia klabu ya FC Liege ya Ubelgiji.

Lommel[hariri | hariri chanzo]

Ilikuwa nchini Ubelgiji ambapo alijitengenezea sifa ambayo ilizindua wasifu wake wa kimataifa. Baada ya msimu mmoja alihamia klabu ya Lommel kutoka klabu ya FC Liege, ambayo sasa ni KVSK United. Alicheza huko kwa muda wa misimu 2 kabla ya kugunduliwa na Club Brugge.

Club Brugge[hariri | hariri chanzo]

Fadiga kwa haraka akawa maarufu kwa mashabiki. maboa 9 katika mechi 67 alizocheza.Mnamo Septemba 2000, kiungo huyu wa kati alirudi Ufaransa na kutia saini mkataba wa AJ Auxerre.

Auxerre[hariri | hariri chanzo]

Akiwa katika klabu hii ya Kifaransa, alishiriki katika mechi 82 za ligi na alifunga mabao 10 na vilevile kushiriki katika kombe la mabigwa barani Ulaya la UEFA na kombe la UEFA wakati wa msimu wa 2002-03.

Internazionale[hariri | hariri chanzo]

Fadiga alihamia Inter Milan katika majira ya joto ya mwaka wa 2003, lakini ugunduzi wa matatizo ya moyo haukumruhusu kushiriki katika mechi za klabu hii ya Kiitaliano, ingawa alicheza mechi kadhaa za kirafiki wakati wa majira ya joto. Aliachiliwa na klabu hiyo ya San Siro baada ya msimu mmoja tu, lakini aliamua dhidi ya kustaafu licha ya matatizo ya moyo.

Bolton Wanderers[hariri | hariri chanzo]

Klabu ya Uingereza ya Bolton Wanderers ilimsaini Fadiga kwa msimu wa 2004-05, baada ya kupasi matibabu. Hata hivyo kabla ya kuchezea Bolton mechi yake ya kwanza, alizirai kabla ya mechi hiyo mwezi wa Oktoba, na aliwekewa mtambo wa “defibrillator” kutokana na mpigo wa moyo ambao haukuwa ya kawaida. Licha ya kusema kuwa alikuwa na hamu kurudi mchezoni, wataalamu wa matibabu walimsihi kustaafu na walimwonya kwamba kama wakati wa mchezo angegongwa kifuani, kulikuwa na uwezekano kwamba mtambo wa “defibrillator” ungeshindwa kufanya kazi, nah hii ingesababisha kifo ya mara moja. Hata hivyo, kufuatia muda wa mapumziko na kupasi matibabu, Fadiga kurejea katika kikosi cha Bolton mapema mwaka wa 2005 na alicheza in mechi 5.

Katika mwanzo wa kampeni ya 2005-06, Fadiga alipeanwa kama mkopo katika klabu ya Derby County ya ligi ya kandanda ya Championship (ligi ya divisheni ya pili) na alicheza mechi nne. Kurudi kwake katika uwanja wa Reebok kulimfanya acheze mechi 10, 2 katika Kombe la UEFA, kabla ya hatimaye kuachiliwa rasmi mnamo Mei 2006 baada ya kushindwa kwa kiasi kikubwa kumfurahisha na kumvutia meneja wa Bolton Sam Allardyce. Mnamo Machi 2006, licha kufunga bao katika sare ya 1-1 dhidi ya Portsmouth FC, pia alikosa mkwaju wa penalti katika mechi hiyo hiyo, [3] hatimaye kugharimu Bolton ushindi ambao ungeiwezesha Boltom kufuzu kushiriki katika kombe la UEFA kwa msimu wa pili mfululizo , sababu ambayo huenda ilifanya mkataba wake kutupiliwa mbali.

Coventry City[hariri | hariri chanzo]

Bila ya kuwa na klabu katika mwanzo wa msimu wa 2006-07, alienda kujaribiwa na klabu ya Portsmouth F.C. na alichezea timu yao hifadhi. Pia alikuwa na majaribu na vilabu vya Watford na Hull City kabla hatimaye kutia saini mkataba wa miezi minne na klabu ya Coventry City tarehe 23 Februari 2007.

Kurudi kwake nchini Ubelgiji[hariri | hariri chanzo]

Tangu wakati huo ameachiliwa na kurejea nyumbani mwa mkewe nchini Ubegiji na kusainiwa na klabu ya AA Gent. Baada ya mwaka mmoja alihamia klabu ya KFC Germinal Beerschot manmo Juni 2008 hadi, lakini aliiacha klabu hiyo ya Beerschot baada ya muda mfupi manmo Desemba 2008

Wasifu wa Kimataifa[hariri | hariri chanzo]

Fadiga aliichezea timu ya kandanda ya taifa ya Senegal mechi zake za kwanza wakati wa msimu wake wa mwisho nchini Ubelgiji. Kwa kuwa alikuwa na pasipoti ya Ubelgiji kupitia ndoa yake, Fadiga alikuwa na uwezo wa kuichezea timu ya kandanda ya taifa ya Ubelgiji, lakini badala yake aliamua kuiwakilisha Senegal na akawa mwanachama muhimu wa timu hiyo ya Senegal katika kampeni za kufuzu kushiriki katika kombe la dunia la mwaka wa 2002 la FIFA na michuano yenyewe,ya ambayo alifunga penalti dhidi ya Uruguay. Senegal walibanduliwa nje ya shindano hilo katika robo fainali na timu ya Uturuki. Bao la ushindi la Uturuki lilifungwa katika muda wa ziada.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Khalilou Fadiga kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.