Kawaka Nzige

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kawaka Nzige alizaliwa na kukulia Bagamoyo nchini Tanzania, Afrika Mashariki ni msanii ambaye yupo tayari kutumia ujuzi wake kuleta manufaa katika jamii na pia kwa sasa yupo nchini Australia kutokana na upendo na kutaka kupanua ujuzi wake juu ya sanaa. [1]

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Alianza kupiga ngoma akiwa bado mdogo katika shule ya msingi na jinsi alivyozidi kukua alifanikiwa kushiriki katika kucheza ngoma na kuimba kwa ajili ya bendi ya Kijiji alichotokea kila siku ya jumamosi usiku ambapo alikua akitumbuiza kwa ajili ya tafrija mbalimbali ndani na nje ya Kijiji alichotokea.

Mnamo mwaka 2007, Kawaka aliweza kuhamia jijini Arusha ambapo huko aliweza kujiunga katika kikundi cha Sanaa ya upigaji ngoma kilichotambulika kwa jina la Kikundi cha asili cha Kucheza ngoma Africa(Africa Traditional Dance Group)kwa Zaidi ya miaka mitano. Katika kikundi hicho Kawaka alifanikisha kuweza kupiga ngoma za asili za makabila na pia kuweza kucheza staili tofauti za ngoma kutoka kwa makabila tofauti tofauti kutoka vijiji mbalimbali Tanzania. Katika kundi hilo la Africa Dace Group, Kawaka alifanikiwa kufanya warsha wa nchi mbalimbali ikiwemo Uswizi, Uholanzi, Ujerumani na Kenya. Pia aliweza kushiriki katika warsha za kusaidia jamii katika kuleta ufahamu kuhusu UKIMWI, kusaidia watoto na pia kupinga unyanyasaji dhidi ya wanawake.

Kwa sasa Kawaka ni mpiga ngoma ambaye anahusishwa na ngoma maarufu ya jadi kutoka katika kabila la kimakonde itokayo kusini mwa Tanzania iitwayo Sindimba. Pasi na kuwa msanii wa muziki wa jadi pia Kawaka ni msanii wa muziki wa taarabu kutokea Zanzibar. [2]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-04-04. Iliwekwa mnamo 2019-04-04. 
  2. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-04-04. Iliwekwa mnamo 2019-04-04. 
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kawaka Nzige kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.