Kasoko ya volkeno
Jump to navigation
Jump to search
Kasoko ya volkeno (pia: kreta kutoka gir./ing. crater) ni shimo kubwa katika mlima wa volkeno.
Zaha na gesi za joto zinapotoka ardhini kuwa volkeno husababisha kutokea kwa kasoko. Milima ya volkeno huwa na kasoko kwenye kelele mara nyingi pia na kasoko kando.
Kasoko za volkeno inayolala au iliyozimika mara nyingi hujaa maji kuwa "ziwa la kasoko".
Shimo linaweza kuonekana kubwa zaidi kama volkeno imeporomoka ndani yake yenyewe halafu huitwa "kaldera".
Kasoko ya volkeno Mount St. Helens (Marekani) baada ya mlipuko wa 1980 - sehemu ya ukingo umepotea
Kasoko za Mlima Kamerun nchini Kamerun
Ziwa ndani ya kaldera (Oregon, Marekani)