Nenda kwa yaliyomo

Kashashi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kashashi ni kata ya Wilaya ya Siha katika Mkoa wa Kilimanjaro, Tanzania, yenye msimbo wa posta 25402.

Kata hiyo inaundwa na vijiji sita: Kirisha, Kyengia, Manio, Lokiri, Kashashi na Naweru.

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 5,573 [1]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 6,694 [2] walioishi humo.

Kashashi ina shule za msingi Kirisha, Suumu, Kyengia, Kittahemwa, Naweru, Lokiri. Pia ina shule ya sekondari moja inayojulikana kwa jina la Suumu Sekondari.

  1. https://www.nbs.go.tz
  2. "Sensa ya 2012, Kilimanjaro - Siha DC" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2004-01-02. Iliwekwa mnamo 2016-05-23.
Kata za Wilaya ya Siha - Mkoa wa Kilimanjaro - Tanzania

Biriri | Donyomurwak | Gararagua | Ivaeny | Karansi | Kashashi | Kirua | Livishi | Makiwaru | Miti Mirefu | Nasai | Ndumeti | Ngarenairobi | Olkolili | Ormelili | Sanya Juu | Songu

Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Kilimanjaro bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Kashashi kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.


Isipokuwa usitaje majina ya viongozi waliopo sasa maana wanabadilika haraka mno.