Kasam Paida Karne Wale Ki

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kasam Paida Karne Wale Ki
Imeongozwa na Babbar Subhash
Imetayarishwa na Babbar Subhash
Nyota Mithun Chakraborty
Smita Patil
Salma Agha
Amrish Puri
Muziki na Bappi Lahiri
Imesambazwa na B. Subhash Film Unit
Imetolewa tar. Novemba 30, 1984 (1984-11-30)
Nchi India
Lugha Kihindi

Kasam Paida Karne Wale Kini filamu iliyotoka mwaka 1984 ya lugha ya [[Kihindi]. Filamu imetayarishwa na kuongozwa na Babbar Subhash. Ndani yake anakuja Mithun Chakraborty, Smita Patil, Salma Agha, Karan Razdan, Geeta Siddharth na Amrish Puri.

Hadithi[hariri | hariri chanzo]

Kasam Paida Karne Wale Ki ni hadithi inayomhusu Satish Kumar (Mithun Chakraborty). Baada ya kifo cha baba yake, Satish anabaki kuwa mrithi pekee wa shamba kubwa kabisa. Kwa vile ana miaka mitano tu, anaruhusiwa kurithi mazima hadi afikapo miaka 20. Shamba hilo lipo chini ya uangalizi wa babake mkubwa, Udaybhan Singh (Amrish Puri), ambaye anamtisha kupindukia mtoto wa kakake kiasi kwamba anaogopa hata kivuli cha babake mkubwa.

Miaka inaenda. Satish anautwaa ukubwa, kamwoa Aarti (Smita Patil), huku bado anaishi maisha ya kumuogopa babake mkubwa. Baada ya usiku mmoja wa furaha, Satish anagundua ya kwamba Aarti alikubali kuolewa nae ili aweze kumwibia fedha taslimu na mikufu ya dhahabu. Anavurugwa. Uday anamtaka Aarti aondoke, halafu Satish anamfuata. Aarti anamwomba msamaha, anamsamehe. Hata hivyo, Udaybhan anampiga kisu cha tumbo hadi kufa na kwenda kuandikisha polisi kama jamaa amaejinyonga. Aarti anaapa kulipiza kisasi kupitia mtoto wake aliyetumboni. Miaka inaenda, Aarti na mtoto wake wa kiume, Avinash (Mithun Chakraborty), anaibuka kulipiza kisasi cha kifo cha Satish — wanagundua sio rahisi kumkaanga Udaybhan, na katika kufanikisha suala zima la kisasi huenda pia likapelekea kuhatarisha maiasha yao.

Washiriki[hariri | hariri chanzo]


Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]