Jye Edwards
Jye Edwards (amezaliwa Machi 6 1998) mwenye asili ya Australia ni mkimbiaji wa umbali wa kati[1]. Edwards alishindana kwenye michezo ya olympiki 2020 Tokyo. Alikuja wa saba kwa joto la Wanaume la 1500m kwa kutumia mda wa 3: 42.62 na kwa hivyo akaondolewa.[2]
Miaka ya awali
[hariri | hariri chanzo]Edwards alianza kushindana akiwa na umri wa miaka 6. Alihimizwa kufanya hivyo pamoja na ndugu zake 3 katika Albion Park klabu ndogo ya riadha, Shellharbour, New South Wales. Alikuwa mchezaji wa kriketi mwenye nia, lakini aligundua kuwa alikuwa mkimbiaji mzuri sana na alijiunga na Klabu ya Riadha ya Michezo ya Bankstown huko Sydney.[3]
Edward ni mwanafunzi wa zamani wa Warilla High School, huko New South Wales na amefundishwa na Dick Telford.[4]
Mafanikio
[hariri | hariri chanzo]Mnamo februari 2017, alirekodi kasi ya saba ya mita 1500 kwenye historia ya Australia huko NSW Juniors Sydney Invitational kwa mda wa 3: 41.69. Alipata maumivu yakupasuka achilles, shida ya goti na kuvunjika kwa mkazo wa femur yake ya kulia kulipunguza kasi ya kazi ya Jye lakini mnamo 2019 alishika nafasi ya pili katika mashindano ya New South Wales Cross Country huko Willandra kwenye sehemu ya open men’s ambapo alionesha kurudi kwake kwenye usawa.[5]
Edwards alikimbia mda wa 7:56 mita 3000 ambapo ilikua ni mda wake bora zaidi huko Sydney mnamo Novemba 2020 na alikimbia tena maili 3:57 bora zaidi mwezi mmoja baadae.[6] Mnamo Aprili 18 2021, Edwards alishinda dhahabu kwenye mda wa 3:33:99 kwenye uwanja wa Sydney Olympiki park ambapo alishinda umbali wa mita 1500 kwenye Mashindano ya Kitaifa ya Riadha ya Australia na kufanikiwa kupata kiwango cha kufuzu cha Olimpiki kwa michezo ya majira ya joto 2020 iliocheleweshwa huko Tokyo.[7] Kukimbia kwenye olympiki huko Tokyo alimaliza nafasi ya saba.[8]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Jye EDWARDS | Profile | World Athletics". www.worldathletics.org. Iliwekwa mnamo 2021-10-09.
- ↑ "Athletics EDWARDS Jye - Tokyo 2020 Olympics". olympics.com (kwa American English). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-10-09. Iliwekwa mnamo 2021-10-09.
- ↑ "Jye Edwards". Australian Olympic Committee (kwa Australian English). Iliwekwa mnamo 2021-10-09.
- ↑ Courtney Ward (2021-06-17). "Edwards ramps up Olympic preparations at Meeting International de Nice". Mandurah Mail (kwa Australian English). Iliwekwa mnamo 2021-10-09.
- ↑ "Nightmare run of injuries ends for star athlete". South Coast Register (kwa Australian English). 2019-06-27. Iliwekwa mnamo 2021-10-09.
- ↑ "WTW: Athing Mu & Jye Edwards Impress, Is Eliud Kipchoge Back or Vulnerable?". LetsRun.com. 2021-04-19. Iliwekwa mnamo 2021-10-09.
- ↑ Thomas Hoogendoorn (2021-04-20). "Canberra runner surges into the Tokyo Olympics". The Canberra Times (kwa Australian English). Iliwekwa mnamo 2021-10-09.
- ↑ "Athletics EDWARDS Jye - Tokyo 2020 Olympics". olympics.com (kwa American English). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-10-09. Iliwekwa mnamo 2021-10-09.