Nenda kwa yaliyomo

June Cohen

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
June Cohen
Picha ya June Cohole akiwa anapokea tuzo ya peabody mwaka 2012
Picha ya June Cohole akiwa anapokea tuzo ya peabody mwaka 2012
Nchi Marekani
Kazi yake [mjasiriamali

June Cohen ni mjasiriamali kutoka Marekani. Kwa sasa ni Mkurugenzi Mtendaji wa WaitWhat, kampuni ya habari aliyoanzisha kwa kushirikiana na Deron Triff. WaitWhat inatengeneza podikasiti ya biashara na fedha kwa kushirikiana na Reid Hoffman, ambaye ni mwanzilishi mwenza wa LinkedIn. Cohen pia alikuwa mwendeshaji wa podikasti Sincerely X katika msimu wake wa kwanza. Mpaka Desemba 2015, alikuwa Mtayarishaji Mtendaji wa vyombo vya habari vya TED (Technology, Entertainment, Design). [1] Aliongoza juhudi za kuleta mkutano huo mtandaoni na  akazindua mfululizo TEDTalks podikasiti  mnamo mwaka  2006, mnamo 2007 TEDTalks iliundwa upya, mnamo 2009 TED ilifungua Mradi wa tafsiri, na manamo mwaka 2010 TED ilifungua mradi wa TV  na Mazungumzo ya TED mnamo 2011.[1]Cohen alijiunga na wafanyakazi wa TED mwaka 2005.[2] Pia alitengeneza saluni za TED za mwaka mzima, alihariri Blogu ya TED,  kushirikiana na kushiriki mkutano wa kila mwaka huko Long Beach, na msimamizi wa TED Chris Anderson. [1][2] Anaishi New York City.[3]

  1. 1.0 1.1 1.2 "Our organization". www.ted.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2022-07-29.
  2. 2.0 2.1 "TEDBios: June Cohen, Director, TED Media". web.archive.org. 2012-07-14. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-07-14. Iliwekwa mnamo 2022-07-29.
  3. Bibliotech Program 2011 speakers Stanford.edu Accessed 2012-07-20 Archived 24 Juni 2016 at the Wayback Machine. iliwekwa manamo 29-07-2022