Jordan Ayew

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Huyu ni Jordan Ayew

Jordan Pierre Ayew (alizaliwa 11 Septemba 1991) ni mchezaji wa soka wa Ghana ambaye anacheza katika klabu ya Crystal Palace iiliyopo Ligi Kuu ya Uingereza kwa mkopo kutoka Swansea City na timu ya taifa ya Ghana. Yeye ni mtoto wa nahodha wa kale wa Ghana Abedi Pele na ndugu wa André Ayew, ambaye anacheza katika klabu ya Fenerbahçe

Kazi ya klabu[hariri | hariri chanzo]

Aston Villa[hariri | hariri chanzo]

Mnamo 27 Julai 2015, Ayew alijiunga na klabu ya Aston Villa kwa mkataba wa miaka mitano(5) kwa ada isiyojulikana, iliyodai kuwa £ 8,000,000.Alifunga goli lake la kwanza katika klabu mnamo 24 Oktoba , 2015 dhidi ya klabu ya Swansea City, dakika ya 62.

Swansea City[hariri | hariri chanzo]

Mnamo 31 Januari 2017, Jordan Ayew alijiunga na klabu ya Swansea City mpaka mwisho wa msimu wa 2019-20 badala ya mlinzi Welsh Neil Taylor,Ndugu bwaba wa Jordan alikuwa mchezaji wa klabu ya Swansea City wakati wa msimu wa 2015-16 na baadaye alijiunga na dirisha la uhamisho la baridi la 2018.

Crystal Palace (mkopo)[hariri | hariri chanzo]

Katika siku ya mwisho ya uhamisho, Ayew alijiunga na klabuy a Crystal Palace kwa mkopo katika msimu wa 2018-19.

Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Jordan Ayew kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.