John Sibi-Okumu

From Wikipedia
Jump to navigation Jump to search

John Sibi-Okumu [www.johnsibiokumu.com] ni mwigizaji Mkenya na mwandishi wa habari anayejulikana kimataifa kwa jukumu lake la uigizaji katika The Constant Gardener Sibi-Okumu alianza kuigiza mwaka 1968 pindi alipokuwa mwanafunzi katika shule ya Lenana, na kuendelea kuchukua hatua mbalimbali katika uigizaji. Ameigiza katika sinema kadhaa, kama vile Born Free (1975), We are the children (1987) na Metamo (1997).[1] Kama mwandishi wa habari, alianzisha kipindi maarufu cha Summit iliyokuwa ikionyeshwa kwa Kenya Television Network (KTN), ambapo yeye aliwahoji wanasiasa wa Kenya. John Sibi-Okumu alizaliwa nchini Kenya. Yeye alianza kusoma nchini Uingereza, (katika shule ya William Pattern School, London) kisha nchini Kenya, (Shule ya msingi ya Muthaiga na Duke York / Shule ya Upili ya Lenana) na hatimaye akaenda Ufaransa (Chuo Kikuu cha Toulouse, "Le Mirail "). Kwa muda mrefu wa maisha yake ya kikazi, alifunza Kifaransa katika shule ya msingi, kati na sekondari, na alikuwa Mkuu wa Idara ya Lugha za Kisasa katika hatua mbalimbali katika kazi ya muda mrefu. Mwaka wa 2002, alipewa taji la kuheshinika la Chevalier des Palmes Académiques, kwa huduma ya Kifaransa na utamaduni nchini Kenya. Mbali na mafanikio yake kama mwalimu, yeye ana sifa ya kuwa mtu wa Sanaa. Kwa miaka mingi iliyopita, amekuwa akijulikana na wasikilizaji na watazamaji nchini Kenya kama mtangazaji wa televisheni na redio. Kwa mfano, kutoka mwaka wa 1997 hadi 2002 kupitia "The Summit," aliwahoji watu maarufu kama Daniel arap Moi, Mwai Kibaki, Robert Mugabe, Ellen Johnson-Sirleaf, Richard Leakey na Wangari Maathai. Hivi karibuni, amekuwa akiuliza maswali katika kipindi cha chemsha bongo "The Celtel Africa Challenge," inayochukua nusu saa nusu saa na inahusu mashindano kati ya wanafunzi wa vyuo vikuu mbalimbali. Msimu wa pili, ulionyeshwa mnamo mwaka 2008 nchini Kenya, Uganda, Tanzania, Malawi na Zambia. Mwaka wa 2009, ilibadilishwa kuwa "The Zain Afrika Challenge," na nchi za Nigeria, Ghana na Sierra Leone ziliongezwa katika orodha ya nchi zinazososhindana. Kuna matarajio ya nchi zingine kuongezeka katika miaka ijayo. Yeye amewahi kusimulia maonyesho mbalimbali zilizoshinda tuzo kwa lugha ya Kiingereza na Kifaransa na ameigiza katika filamu kadhaa, miongoni mwao kwenye tamthiliya kama Waziri wa Afya Dr Yoshua Ngaba katika "The Constant Gardener" iliyoshinda tuzo la Oscar na kwenya maisha halisi kama mwanadiplomasia wa Shirika la Umoja wa Mataifa, Jacques Roger Boh-Boh, katika "Shake Hands with the Devil," hadithi ya mauaji ya kimbari ya Rwanda kupitia kwa Romeo Dallaire, ambaye ans asili ya Kifaransa na Canada. Katika miaka iliyopita, ameigiza katika majukumu ya kustaajabisha kama Mfalme Oedipus; Romeo, Oberon and Shylock (Shakespeare); Anouilh Creon katika "Antigone," Beckett Vladimir katika "Waiting for Godot and Mtwa / Ngema' s Percy katika" Woza, Albert! " Yeye mwenyewe ameanzisha "In Search of the Drum Major" na "Like Ripples On a Pond," zote juu ya haki za binadamu (American Civil Rights Movement), na pia "Milestones," '

"Showcase"[edit | edit source]

Yeye ameandika michezo miwili ya awali kabisa: Ya kwanza, "Role Play - A Journey into Kenyan Psyche," iliyochapishwa mwaka 2005 (Mvule Africa Publishers; ISBN 9966-769-42-0) iliyochambuliwa na Newsweek International kama "mtazamo wa ubaguzi wa kirangi nchini Kenya ambao hauhitaji msamaha." Mchezo wa pili ni, "Minister ... karibu!" iliyotizamwa mjini Nairobi na watazamaji tarehe Oktoba 2007 na itachapishwa tena baada ya kuandikwa tena. Katika "Minister .... Karibu!" Sibi-Okumu anatumia kinaya, kuwaonyesha Wakenya hatari ya ubinafsi wa kisiasa na jinsi inavyoharibu utulivu wa kijamii. Ameandika kitabu kingine "Tom Mboya: Master of Mass Management," kwa ajili ya wasomaji wachanga, iliyochapishwa na (Sasa Sema / Longhorn Publishers: ISBN 978-9966-36-328-9). Mwezi Oktoba 2009 John Sibi-Okumu [5] alijihusisha katika kutengeneza filamu ya kimuziki Mo Faya, iliyoonyeshwa katika New York Theatre Festival 2009. Yeye kama mwandishi wa habari ameandika taarifa tofauti kwa magazeti na majarida ya Kenya kwa kutumia jina la kujibandikiza la Mwenye Sikio na, kwa miaka mitatu, alikuwa kwenye bodi ya kuhariri ya jarida la "AWAAZ-Voices of the South Asian Diaspora," ([www.awaazmagazine.com ]), ambayo anaendelea kuandika mara kwa mara iitwayo: "Alternative Angle." Kuongezea yote hayo, amekuwa akifanya kazi kama mhariri, akijihusisha mara nyingi na utafiti wa kisayansi. Katika maisha yake ya utu uzima, John Sibi-Okumu daima hukaribishwa fursa kwa kukopesha talanta yake kwa hisani na katika ustawi wa jamii.

Marejeo[edit | edit source]

[www.johnsibiokumu.com]

  1. [0] ^ Anthony Njagi, "In celebration of Black History Month", Weekend Magazine, 18 Januari 2002

Viungo vya nje[edit | edit source]

[www.johnsibiokumu.com]

Viungo vya ndani[edit | edit source]

John Sibi-Okumu