John Okafor

John Ikechukwu Okafor (maarufu kama Mr. Ibu, 17 Oktoba 1961 – 2 Machi 2024) alikuwa mwigizaji nguli na mchekeshaji kutoka Nigeria.Alionekana katika filamu zaidi ya 200 za Nollywood ikiwa ni pamoja na zile za mfululizo wa Mr. Ibu.
Maisha ya awali na elimu
[hariri | hariri chanzo]Okafor alizaliwa mnamo 17 Oktoba 1961. Alitoka Umunekwu katika Mkoa wa Mashariki wa zamani wa Nigeria (sasa katika Nkanu West L.G.A., Enugu State).[1] Baada ya shule ya msingi na kifo cha baba yake mnamo mwaka 1974, Okafor alihamia Sapele kuishi na kaka yake. Huko Sapele, alifanya kazi ndogo ndogo ili aweze kujiandikisha shuleni na kusaidia familia yake.[2] Baadaye alifanya kazi kama mpamba nywele, akaingia kwenye upigaji picha na pia kufanya kazi katika kampuni inayotengeneza makontena. Baada ya shule ya sekondari, alikubaliwa kwenye Chuo cha Elimu, Yola, lakini aliondoka kutokana na changamoto za kifedha. Baadaye aliendelea na masomo katika Institute of Management and Technology (IMT), Enugu. Alifanya kazi kama mpamba nywele, akaingia kwenye upigaji picha na pia kufanya kazi katika kampuni inayotengeneza makontena.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Okoth, Brian (2 Machi 2024). "'Mr Ibu': Veteran Nigerian actor John Okafor dies at 62". TRT Afrika (kwa Kiingereza).
{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Momoh, Mohammed (3 Machi 2024). "Mr Ibu, Nigerian actor who cracked African ribs, dies at 62". Nation (kwa Kiingereza).
{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
| Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu John Okafor kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |