Nenda kwa yaliyomo

Johan Cruyff

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Johan Cruyff

Hendrik Johannes "Johan" Cruijff (ilibadilishwa kuwa Cruyff; 25 Aprili 194724 Machi 2016) alikuwa gwiji mchezaji na kocha. Alipokuwa mchezaji alishinda Ballon d'Or mara tatu mwaka 1971, 1973, 1974.

Cruyff alikuwa wa kwanza kuweza kutumia falsafa ya Total Football iliyoundwa na Rinus Michels, na anajulikana kama mchezaji bora wa soka kuwahi kutokea katika historia ya soka.Katika miaka ya 1970 mpira wa Uholanzi uliibuka na kuwa na ushindani kwenye michuano.

Cruyff aliisaidia Uholanzi kufika kwenye fainali za kombe la dunia mwaka 1974 na kupewa mpra wa dhahabu kama zawadi kwa mchezaji bora kwenye mashindano.Kwenye fainali ya 1974 alifanya mashambulizi yaliyoitwa "Cruyff Turn" ambao ni mfumo unaotumika kwa sasa.Katika ngazi ya klabu alianza kucheza na Ajax, na alishinda Eredivisie mara nane, European Cups mara tatu na Intercontinental Cup mara moja.

Mwaka 1973 alihamia Barcelona kwa kuvunja rekodi ya usajili, msimu wake wa kwanza alishinda taji la La Liga na kuitwa mchezaji bora wa Ulaya wa mwaka. Baada ya kustaafu mwaka 1984, Cruyff alikuwa kocha mwenye mafanikio makubwa wa Ajax na baadaye Barcelona baadaye alikuwa mshauri wa klabu zote mbili.

Mwanaye Jordi pia alicheza soka.

Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Johan Cruyff kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.