Nenda kwa yaliyomo

Johannesburg

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Jiji la Johannesburg)






Jiji la Johannesburg

Bendera

Nembo
Jiji la Johannesburg is located in Afrika Kusini
Jiji la Johannesburg
Jiji la Johannesburg

Mahali pa mji wa Johannesburg katika Afrika Kusini

Majiranukta: 26°11′24″S 28°2′24″E / 26.19000°S 28.04000°E / -26.19000; 28.04000
Nchi Afrika Kusini
Majimbo Gauteng
Tovuti:  www.joburg.org.za
Kitovu cha mji wa Johannesburg
Kitovu cha mji wa Johannesburg

Johannesburg (inayojulikana pia kama iGoli) ni jiji kubwa katika nchi ya Afrika Kusini. Ni mji mkuu wa jimbo la Gauteng.

Mji ulianzishwa 4 Oktoba 1886 ukakua haraka baada ya kupatikana kwa dhahabu. Siku hizi ni kitovu cha kiuchumi wa Afrika Kusini na makao ya soko la hisa kubwa katika Afrika.

Japokuwa johannesburg ni mji mkubwa lakini sio miongoni mwa miji mikuu mitatu ya Afrika Kusini lakini mahakama ya katiba inakaa hapa.

Pia kuna jengo lililosheheni maofisi kubwa kuliko yote barani Afrika ambalo linaitwa Carlton Centre lenye ghorofa 50 kuna pia jengo refu kabisa barani afrika linaloitwa Hillbrow Tower (mita 270 au maghorofa 90).

Karibu theluthi moja ya wakazi wa jiji la johannesburg huishi katika eneo la Soweto ambalo ni mtaa maarufu ulioengwa nje ya jiji asilia kwa ajili ya wafanyakazi Waafrika wakati wa Apartheid (siasa ya ubaguzi wa rangi). Jozi kama inavyojulikana na wengi ni moja kati ya miji mikubwa duniani iliyoendelea(kujengeka) sehemu ambako hakuna mto,ziwa ama bahari ufukwe..! Imehaririwa na Selemani Mkonje

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika Kusini bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Johannesburg kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.