Nenda kwa yaliyomo

Jennifer Bash

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jennifer Bash
Jina la kuzaliwa Jennifer Bash
Nchi Tanzania
Kazi yake Mjasiriamali wa kilimo
Ndoa Innocent Bashungwa

Jennifer Bash ni mwanamke mjasiriamali katika kilimo nchini Tanzania, mwanzilishi wa kampuni AKTZ Industries Ltd inayojihusisha na utengenezaji wa vyakula vyenye chapa ya Alaska Tanzania[1].

Kutokana na jitihada zake katika ujasiriamali, alifanikiwa kuzawadiwa tuzo na kampuni ya utangazaji ya Clouds Media Group mwaka 2016 kama mwanamke aliyefanikiwa katika biashara ya kilimo.