Isimu
Mandhari
Isimu (au "maarifa ya lugha") ni sayansi inayochunguza lugha. Imegawiwa katika matawi mbalimbali:
- fonetiki kuhusu sauti zinazotolewa na binadamu
- fonolojia kuhusu mfumo wa sauti katika lugha fulani
- mofolojia kuhusu mfumo wa maneno
- sintaksi kuhusu mfumo wa sentensi
- semantiki kuhusu maana
- isimujamii kuhusu uhusiano kati ya lugha na jamii
Marejeo
- TUKI 1990, "Kamusi Sanifu ya Isimu na Lugha", Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
- Massamba, David 2004, "Kamusi ya Isimu na Falsafa ya Lugha", Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
Tazama pia
Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Isimu kama historia yake, uenezi au maendeleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |