Ischemia
Ischemia | |
---|---|
Mwainisho na taarifa za nje | |
Matamshi | |
Kundi Maalumu | Upasuaji wa Mishipa ya Damu |
Miaka ya kawaida inapoanza | Polepole au ghafla[3] |
Visababishi | Polepole: Ugumu na wembamba wa mishipa, ukuaji usio wa kawaida wa seli kwenye kuta za mishipa, kuvimba kwa mishipa ya damu, uvimbe[3] Ghafla: damu iliyoganda, kujibana kwa ghafla kwa mishipa ya damu, kupasuka kwa aorta[3][4] |
Ischemia ni kizuizi cha usambazaji wa damu kwenye tishu na kusababisha upungufu wa oksijeni.[3] Aina zake ni pamoja na ugonjwa wa moyo wa ischemia, kiharusi, ugonjwa wa mishipa ya pembeni na mesenteric ischemia.[5] Dalili zake hutegemea eneo la mwili lililoathirika.[5] Kuanza kwake kunaweza kuwa polepole au ghafla.[3]
Matukio ya polepole yanaweza kutokea kutokana na ugumu na wembamba wa mishipa ya damu kutokana na tauni (atherosclerosis), ukuaji usio wa kawaida wa seli kwenye kuta za mishipa unaoweza kusababisha kuziba kwake (fibromuscular dysplasia), kuvimba kwa mishipa ya damu kunakoweza kuzuia mtiririko wa damu na kuharibu viungo na tishu (vasculitis), au shinikizo la nje kutoka kwa uvimbe.[3] Matukio ya ghafla zinaweza kutokea kwa sababu ya kuganda kwa damu, kujibana kwa ghafla kwa mishipa ya damu kunakopunguza mtiririko wa damu (vasospasm), au tabaka za ndani za aota kukatika na kusababisha mtiririko wa damu kati ya tabaka za ukuta wa aota.[3][4]
Juhudi za kuzuia hali hiyo ni pamoja na maisha yenye afya nzuri.[5] Matumizi ya kwanza yaliyoandikwa katika kumbukumbu ya neno hili ni kutoka mwaka wa 1855.[2] Neno hili linatokana na neno la Kigiriki ischein linalomaanisha "kuzuia" pamoja na haima ambalo maana yake ni "damu".[2]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Martin, Elizabeth A. (1987). Concise Medical Dictionary (kwa Kiingereza). Oxford University Press. uk. 107. ISBN 978-0-19-281991-8. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-04-27. Iliwekwa mnamo 2016-05-15.
- ↑ 2.0 2.1 2.2 "Definition of ISCHEMIA". www.merriam-webster.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 26 Januari 2021. Iliwekwa mnamo 27 Februari 2021.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 3.0 3.1 3.2 3.3 3.4 3.5 3.6 "Occlusive Peripheral Arterial Disease - Heart and Blood Vessel Disorders". Merck Manuals Consumer Version. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 19 Machi 2021. Iliwekwa mnamo 27 Februari 2021.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 4.0 4.1 Hotchkiss, R; Marks, T (Machi 2014). "Management of acute and chronic vascular conditions of the hand". Current reviews in musculoskeletal medicine. 7 (1): 47–52. doi:10.1007/s12178-014-9202-6. PMID 24668045.
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 5.0 5.1 5.2 "What Is Ischemia?". WebMD (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 1 Machi 2021. Iliwekwa mnamo 27 Februari 2021.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Ischemia kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |