Nenda kwa yaliyomo

Ingeborg Schwenzer

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Ingeborg Schwenzer (aliyezaliwa tarehe 25 Oktoba 1951 jijini Stuttgart, Ujerumani) ni msomi wa sheria wa kijerumani na profesa wa sheria za ulinganifu katika Chuo Kikuu cha Basel, Switzerland.

Maelezo Binafsi (Curriculum Vitae)

[hariri | hariri chanzo]

Ingeborg Schwenzer alisomea sheria katika Chuo Kikuu cha Freiburg i. Br. na Chuo Kikuu cha Université de Genève kati ya mwaka 1970 na mwaka 1975. Kuanzia mwaka 1973 hadi 1975 alifanya kazi kama mwanafunzi msaidizi katika Taasisi ya sheria za utawala katika Chuo Kikuu cha Freiburg i. Br.

Mwaka 1975 , Schwenzer alifaulu mtihani wa Erste juristische Staatsprüfung (First State Exam in Law) katika Chuo Kikuu cha Freiburg na kushika nafasi ya tatu (3) kati ya watahiniwa 209.

Kuanzia mwaka 1975 hadi 1976, Schwenzer alisoma katika Chuo Kikuu cha Carifornia, Berkeley na kutunukiwa shahada ya uzamili katika sheria yenye heshima.

Kuanzia mwaka 1977 hadi 1981, Schwenzer alikuwa mtafiti msaidizi wa Peter Schlechtriem katika Taasisi ya Sheria za kimataifa na ulinganifu katika Chuo Kikuu cha Freiburg. Mwaka 1978 alitunukiwa shahada ya uzamili ( Dr. iur. utr.) kwenye andiko lake Die Freizeichnung des Verkäufers von der Sachmängelhaftung im amerikanischen und deutschen Recht (The seller’s limitation of liability for defective goods under American and German law). Andiko lake lilipata tuzo ya Herrnstadt kwa kuwa andiko bora kwa mwaka 1978.

Kuanzia mwaka 1978 hadi 1980, Schwenzer alifanya mafunzo ya sheria kwa vitendo katika Chuo Kikuu cha Freiburg i. Br. na kufaulu mtihani wa Zweite juristische Staatsprüfung (Second State Exam in Law) ambapo alishika nafasi ya kwanza kati ya watahiniwa 334.

Kati ya mwaka 1980 na mwaka 1987, Schwenzer alikuwa msaidizi profesa na mhadhiri wa sheria za biashara katika Verwaltungs- und Wirtschaftsakademie (Academy of Administration and Commerce) katika Chuo Kikuu cha Freiburg i. Br.

Mwaka 1986, Schwenzer aliteuliwa kuwa mhadhiri kwenye Chuo Kikuu cha Philipps-Universität Marburg.

Mwaka 1987, andiko la Schwenzer lenye kichwa Vom Status zur Realbeziehung – Familienrecht im Wandel (From status to actual relation – family law in the flux) lilikubaliwa na Chuo Kikuu cha Freiburg na kutunukiwa venia legend kwenye sheria za masuala binafsi, sheria za biashara, sheria za kimataifa na sheria za ulinganifu. Baadaye alikuwa profesa mbadala wa kwenye sheria za masuala binafsi, sheria za biashara, sheria za kimataifa, sheria za ulinganifu na sheria za kazi katika Chuo Kikuu cha Konstanz. Baadaye aliombwa na Chuo Kikuu cha Köln kuwa profesa wa sheria za masula binafsi na hapohapo akaombwa na Chuo Kikuu cha Mainz kuwa profesa wa sheria za masuala binafsi, sheria za kimataifa na sheria za ulinganifu. Alikubaliana na maombi ya Chuo Kikuu cha Mainz na kuteuliwa kuwa profesa mwezi Desemba 1987.

Mwaka 1989, Schwenzer alipewa cheo cha uprofesa kwenye kiti cha sheria za masuala binafsi katika chuo Kikuu cha Basel. Baadaye alipewa nafasi na Chuo Kikuu cha Kiev kuwa profesa wa sheria za masuala binafsi za Ujerumani na Jumuiya ya Ulaya na pia aliombwa Chuo Kikuu cha Humboidt,Berlin (1995) kuwa profesa wa sheria za masuala binafsi. Maombi yote aliyakataa. Kwa mwaka 2107, alistaafu kutoka chuo kikuu cha Basel.

Tangu mwaka 2010 hadi mwaka 2016, Schwenzer anafanya kazi ya ziada kama profesa kwenye Chuo Kikuu cha City Hong Kong tangu mwaka 2010 hadi 2016 na chuo kikuu cha Griffith, Australia, tangu mwaka 2013 hadi 2016.

Tangu mwaka 2014 Schwenzer wa (SiLS) - Swiss International Law School

Kwa miaka mingi, Schwenzer alikuwa profesa mwalikwa kwenye taasisi mbalimbali: 1994 – 2002 katika Europainstitut, Basel, Switzerland; mwaka 2008 katika Chuo kikuu cha Paris Val-de-Marne, France; mwaka 2009 katika Chuo Kikuu cha Victoria Wellington, New Zealand; mwaka  2010 katika Chuo Kikuu cha  Loyola Chicago, USA; mwaka 2011 katika Chuo Kikuu cha  Buea, Cameroon; na pia mwaka 2011 katika Chuo Kikuu cha İstanbul Bilgi, Turkey 2012 katika chuo kikuu cha Ankara,Turkey, pia Katika mwaka 2012 chuo kikuu cha Pontifícia Universidade Católica do Paraná,Brazil, Katika mwaka 2013 chuo kikuu cha Universitetet i Oslo, Norway ; mwaka 2014 katika chuo kikuu cha Griffith, Australia; mwaka 2015 katika chuo kikuu cha Dar el-Hekma, Jeddah, Saudi Arabia.

Maeneo anayopendelea kufanyia Utafiti

[hariri | hariri chanzo]

Katika utafiti wake, Schwenzer anapendelea anaangalia zaidi kwenye sheria za uwajibikaji , sheria za biashara na sheria za familia. Aidha, anapendelea masuala ya usuluhishi.

Sheria za mauzo ulimwenguni

[hariri | hariri chanzo]

Mradi wa sheria za mauzo ulimwenguni unahusu ulinganifu wa sheria za mauzo na sheria za mikataba.

Sheria za mauzo ulimwenguni na Sheria za mikataba

[hariri | hariri chanzo]

Kiini cha mradi huu ni kijitabu kinachoitwa Global Sales and Contract Law (GSCL)[1], ambacho Schwenzer aliandika kwa kushirikiana na Pascal Hachem na Christopher Kee. Kijitabu hiki kinalinganisha sheria zinazosimamia mauzo na mikataba katika zaidi ya nchi 60. Waandishi wa kitabu hiki walitumia maandiko ya shahada za uzamivu za Mohamed Hafez (Uarabuni na Mashariki ya Kati), Natia Lapiashvili (Ulaya Mashariki na Asia ya Kati), Edgardo Muñoz (Amerika ya Kilatini), Jean Alain Penda Matipe (Kusini ya Jangwa la Sahara), na Sophia Juan Yang (Asia ya Kusini Mashariki).Kila andiko lilihusu ulinganifu wa mfumo wa sheria wa aina moja ya na zilisimamiwa na Schwenzer.

Maoni kwenye jarida la CISG

[hariri | hariri chanzo]

Schwenzer anahariri jarida linaloongoza kutoa maoni juu ya the UN Convention on Contracts for the International Sale of Goods (CISG). Jarida hili lilichapishwa kwenye lugha ya Kijerumani (Toleo la 6 mwaka 2013)[2], Kiingeleza (Toleo la 4 mwaka 2016)[3], [3]Kispaniola (mwaka 2011)[4]. Kireno (2014), Kituriki (2015), kifaransa, kichina, kirusi na matoleo zaidi zinaendelea.

CISG-online.ch

[hariri | hariri chanzo]

Mpaka kustaafu kwake kwa mawaka 2017 Schwenzer anaendesha mtandao wenye taarifa za kina kuhusu kesi muhimu kuhusu CISG. Mtandao huu umeenea kwenye nchi zinazoongea lugha[5] ya kijerumani. Mtandao huu ulianzishwa mwaka 1995 na Peter Schlechtriem katika Chuo Kikuu cha Freiburg i. Br. Tangu mwaka 2002 ilikuwa unasimamiwa  na Schwenzer katika Chuo Kikuu cha Basel tangu mwaka 1995 hadi mwaka 2015.

Willem C. Vis International Commercial Arbitration Moot

[hariri | hariri chanzo]

Tangu kuanza kwa mashindano ya usuluhishi ya Willem C. Vis Moot mwaka 1994, Schwenzer amekuwa akishiriki kwenye nafasi ya msuluhishi katika mashindano haya ambayo hufanyika Vienna kila mwaka na ambayo ni mashindano makubwa ya aina hii duniani. Tangu mwaka 2004 ameshiriki pia kama msuluhishi kwenye mashindano ya Willem C. Vis East Moot yanayofanyikia Hong Kong. Aidha, tangu mwaka 1995 amekuwa anaandaa timu ya Chuo Kikuu cha Basel kwenye mashindano ya Vis.

Model Family Code

[hariri | hariri chanzo]

Kwenye mwaka 2006, Schwenzer aliaandaa rasimu ya kuunganisha sheria za familia, inayoitwa the Model Family Code[6], kwa kushirikiana na Mariel Dimsey. Ulinganifu wa kina kwenye sheria za familia za Ulaya, Amerika na Oceania ndio ulioweka msingi wa kuandaa Model Family Code . Faida ya Model Family Code na sheria za kifamilia za nchi zingine ni kwamba inajumuisha mambo muhimu katika sheria za kifamilia. Aidha, Model Family Code inaruhusu kuzingatia masuala ya utamaduni katika sheria za kifamilia.

SiLS-Swiss International Law School

[hariri | hariri chanzo]

Schewenzer ni Mkuu wa Swiss International Law School (SiLS) Ilihifadhiwa 22 Februari 2017 kwenye Wayback Machine., binafsi mtandao msingi shule ya sheria sadaka mpango LL.M

Machapisho muhimu na Uhariri

[hariri | hariri chanzo]

Kwa mujibu wa orodha ya machapisho ya  Schwenzer iliyotolewa (kama ya Februari 2017)[7], Schwenzer ametoa machapisho binafsi 17, ama haridi zaidi ya vitabu 40, na kuandikwa makala zaidi ya 200 na michango ya fafanuzi.

Kwa orodha ya kina ya uanachama: https://www.ingeborgschwenzer.com/publications

Uanachama katika jumuiya mbalimbali

[hariri | hariri chanzo]

·        Tangu mwaka 2016 mwanzilishi mwanachama wa kiengo cha chuo cha utatuzi wakimataifa.

·        Tangu mwaka 2015 mwanachama wa taasisi yasheria ya kimarekani.

·        Tangu mwaka 2014 Bodi ya Wakurugenzi wa Chuo cha Kimataifa cha Sheria ya biashara na matumizi vya mwanachama.

·        Tangu mwaka 2013 mwanachama wa bodi ya jamii sheria ya kimataifa ya ujeremani.

·        Tangu 2011 mwenyekiti wa baraza la ushami wa CISGC (Convention on Contracts for the International Sale of Goods) Advisory Council.

·        Tangu mwaka 2011 mwanachama wa chama cha sheria ya kimataifa, tawi la Swiss.

·        Tangu mwaka 2010 mwanachama wa chuo cha sheria ya ulaya

·        Tangu mwaka 2010 mwanachama wa Baraza la Taasisi ya Usuluhishi Mashirika ya Kimataifa ya kielimu

·        2004-2012 Naibu Mwenyekiti wa Bodi ya Ujerumani ya chama ya wanasheria

·        Tangu mwaka 2001 Mwanachama wa Kundi Mtaalam wa Tume ya Sheria za familia Ulaya

·        Tangu mwaka 2000 mwanachama wa Chuo cha Kimataifa cha Sheria ya kulinganisha

·        1999-2005 mwanachama wa Bodi ya Chama cha wahadhiri katika Sheria binafsi (Zivilrechtslehrervereinigung)

·        1993-2006 mwanachama wa wa bodi la Taasisi ya Sheria ya kulinganisha Swiss

  • Mwaka 2011 alipata tuzo ya “Law Career Achievement Award” ya Chama cha Waarabu kwenye Sheria za biashara na bahari.
  1. http://lccn.loc.gov/2011939853
  2. http://d-nb.info/989417662
  3. http://d-nb.info/999239821
  4. http://www.worldcat.org/title/schlechtriem-schwenzer-comentario-sobre-la-convencion-de-las-naciones-unidas-sobre-los-contratos-de-compraventa-internacional-de-mercaderias/oclc/754653801&referer=brief_results
  5. "Overview - Global Sales Law Project - Deutsch - A Comparison of the CISG, International and Nationals Sales Laws". Globalsaleslaw.org. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-03-04. Iliwekwa mnamo 2013-08-11.
  6. "Model Family Code : Form a global perspective / Ingeborg Schwenzer" (kwa Kijerumani). //d-nb.info. Iliwekwa mnamo 2013-08-11. {{cite web}}: External link in |publisher= (help)
  7. Publications Ingeborg Schwenzer

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]