Inesha

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Inesha (kutoka Kilatini inertia) ya gimba fulani ni tabia ya masi kubaki katika hali yake ya kutulia au kuwa na mwendo fulani hadi iathiriwe na nguvu ya nje.

Masi kubwa zaidi huwa na inesha kubwa zaidi na inahitaji nguvu kubwa zaidi kwa kubadilisha mwendo wake. Tunaiona kwa urahisi tukijaribu kusukuma baisikeli, gari au lori: masi zake ni tofauti, hivyo nguvu inayohitajika kuzisukuma au kuzisimamisha inatofautiana.

Makala hii kuhusu mambo ya fizikia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Inesha kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.