Indinaviri
Mandhari
Indinaviri (Indinavir (IDV)), inayouzwa kwa jina la chapa Crixivan, ni dawa inayotumika kutibu HIV/UKIMWI pamoja na dawa nyingine[1], lakini sio matibabu ya mstari wa kwanza.[1] Dawa hii inachukuliwa kwa mdomo.[1]
Madhara yake ya kawaida ni pamoja na kichefuchefu, maumivu ya tumbo, maumivu ya kichwa, na mawe kwenye figo.[1] Madhara yake mengine yanaweza kujumuisha matatizo ya ini, kisukari na ugawaji tena wa mafuta mwilini.[1] Usalama wa matumizi yake katika ujauzito hauko wazi.[2] Ni kizuizi cha protease.[1]
Indinaviri ilipewa hati miliki mwaka wa 1991 na kuidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya kimatibabu nchini Marekani na Ulaya mwaka wa 1996.[3][1][4] Nchini Marekani, inagharimu takriban Dola 450 kwa mwezi kufikia mwaka wa 2021.[5]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 1.5 1.6 "Indinavir Monograph for Professionals". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 24 Agosti 2021. Iliwekwa mnamo 26 Novemba 2021.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Indinavir (Crixivan) Use During Pregnancy". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 28 Novemba 2020. Iliwekwa mnamo 26 Novemba 2021.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Fischer, Jnos; Ganellin, C. Robin (2006). Analogue-based Drug Discovery (kwa Kiingereza). John Wiley & Sons. uk. 509. ISBN 9783527607495. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-06-20. Iliwekwa mnamo 2021-08-05.
- ↑ "Crixivan". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 15 Aprili 2021. Iliwekwa mnamo 26 Novemba 2021.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Indinavir Sulfate Prices, Coupons & Savings Tips - GoodRx". GoodRx. Iliwekwa mnamo 26 Novemba 2021.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)