Idara ya Usalama wa Taifa (Tanzania)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Idara ya Usalama wa Taifa Tanzania (kwa Kiingereza Tanzania Intelligence and Security Service; kifupi: TISS) ni idara ya usalama nchini Tanzania.[1]

Idara hiyo inafanya kazi kwa karibu na mashirika mengine ya kitaifa na ya kimataifa katika nyanja za kiusalama katika kuhakikisha amani ya kudumu, ulinzi na usalama, vinapatikana ndani na nje ya mipaka ya Tanzania.

Wachambuzi mbalimbali wamechapisha juu ya ufanyiaji wa mabadiliko katika idara hii, ikiwepo kutangaza nafasi za kazi kwa wazi kama ambavyo vyombo vingine vya ulinzi na usalama nchini na duniani hufanya.

Kwa muktadha huo ni chombo ambacho kina kazi sawa na Uhamiaji ambapo hufanya kazi ya kulinda amani pamoja na mipaka ya nchi.

Ukitoa usalama ambao ni kazi ya serekali, ni jukumu la kila mwananchi kulinda amani ya nchi na kutoa taarifa ya jambo lolote linaloashiria uvunjifu wa amani ama ukiukaji wa haki stahiki za uingiaji nchini.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. The Tanzania Intelligence and Security Service Act, 1996. Parliament of Tanzania (1996). Jalada kutoka ya awali juu ya 2013-09-27. Iliwekwa mnamo 16 September 2013.