Idara ya Usalama wa Taifa (Tanzania)
Mandhari
Idara ya Usalama wa Taifa Tanzania (kwa Kiingereza Tanzania Intelligence and Security Service; kifupi: TISS) ni idara ya usalama nchini Tanzania.[1]
Idara hiyo inafanya kazi kwa karibu na mashirika mengine ya kitaifa na ya kimataifa ya nyanja za usalama katika kuhakikisha amani ya kudumu, ulinzi na usalama, vinapatikana ndani na nje ya mipaka ya Tanzania.
Kwa muktadha huo ni chombo ambacho kina kazi sawa na Idara ya Uhamiaji ambapo hufanya kazi ya kulinda amani pamoja na mipaka ya nchi.
Ukitoa usalama ambao ni kazi ya serikali, ni jukumu la nchi na viongozi wa idara hizo mbili kutoa taarifa ya jambo lolote linaloashiria uvunjifu wa amani ama ukiukaji wa haki stahiki za uingiaji nchini.
Wakurugenzi wa Idara ya Usalama wa Taifa (Tanzania)
| Na | Jina | Muda aliohudumu | Maelezo |
|---|---|---|---|
| 1 | Emilio Mzena | 1961–1975 | Mkurugenzi wa kwanza baada ya kupata uhuru; alichagulia na Rais Julius Nyerere. |
| 2 | Dr. Lawrence Gama (PhD) | 1975–1978 | Baadaye alichaguliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma. |
| 3 | Dr. Hassy Kitine (PhD) | 1978–1980 | Mteule kijana zaidi; alihusika hasa upande wa usalama kipindi cha Vita vya Kagera.[2] |
| 4 | Dr. Augustine Mahiga (PhD) (Alikaimu) | 1980–1983 | Baadae alihudumu kama Balozi na Mwanadiplomasia wa Umoja wa Mataifa. |
| 5 | Lt. Gen. Imrani Kombe | 1983–1995 | Alifariki mnamo mwaka 1996. |
| 6 | Col. Apson Mwang’onda | 1995–2005 | Aliboresha na kuunda upya mfumo wa TISS. |
| 7 | Othman Rashid | 2005–2016 | Alihudumu kipindi chote cha utawala wa Rais Jakaya Kikwete. |
| 8 | Dr. Modestus Kipilimba (PhD) | 2016 – 12 Sept 2019 | Alichaguliwa na Rais John Pombe Magufuli. |
| 9 | CP Diwani Athumani Msuya | 12 Sept 2019 – 3 Jan 2023 | Alikua Kamishina wa Polisi. |
| 10 | Said Hussein Massoro | 3 Jan 2023 – ~Aug 2023 | Alihudumu kwa kipindi kifupi cha miezi 8. |
| 11 | Balozi Ali Idi Siwa | Aug 2023 – 11 July 2024 | Alihudumu kwa muda wa miezi 11 na kustaafu. |
| 12 | Suleiman Abubakar Mombo | 11 July 2024 – Mpaka sasa | Alichaguliwa na Rais Samia Suluhu Hassan.[3] |
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "The Tanzania Intelligence and Security Service Act, 1996" (PDF). Parliament of Tanzania. 1996. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2013-09-27. Iliwekwa mnamo 16 Septemba 2013.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ https://www.bing.com/search?pglt=931&q=Dr.+Hassy+Kitine&cvid=64a720e9777b46b5b08df6a648a84ab5&gs_lcrp=EgRlZGdlKgYIABBFGDkyBggAEEUYOdIBBzgyNmowajGoAgCwAgA&FORM=ANNTA1&PC=U531
- ↑ "President Samia appoints new spy chief". The Citizen. 2024-07-11. Iliwekwa mnamo 2025-08-15.
| Makala hii kuhusu mambo ya siasa bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Idara ya Usalama wa Taifa (Tanzania) Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |