Nenda kwa yaliyomo

Humanium

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kichezeo kilichotengenzwa kwa humanium

Humanium ni jina kwa aloi ya feleji inayotengenezwa kwa kuyeyusha bunduki haramu zinazokamatwa katika maeneo penye jinai au mvurugo katika Amerika ya Kati, Marekani au Afrika[1]. "Humanium metal" inamaanisha "metali ya kiutu", kama kinyume cha "metali ya silaha".

Silaha ambazo kwa kawaida zilikamatwa na serikali mbalimbali zinanunuliwa na shirika lisilo la faida la Individuell Människohjälp kutoka Uswidi na kuharibiwa kwa kuzikatakata. Baadaye zinapashwa moto hadi kuyeyuka. Vipande vya feleji vinatumwa Uswidi na huko kuna kampuni inayotengeneza unga wa chuma au moja kwa moja vifaa vinavyoweza kuuzwa kama vile saa, kalamu na viatu. Faida kutokana na biashara hii hutumiwa katika maeneo penye mvurugo kwa miradi ya kujenga amani na kusaidia wahanga[2].

Madhumuni yaliyotajwa ya kampeni hiyo ni kulenga masuala ya unyanyasaji wa bunduki na kuchangia katika kukomesha biashara haramu ya silaha [3].

  1. Humanium Is A Metal Made From Guns, To Help Stop Gun Violence
  2. Pangburn, D. J. (2019-01-03). "How watches made of seized guns can help rebuild El Salvador's economy". Fast Company (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2020-01-19.
  3. "Humanium Metal". humanium-metal.com. Iliwekwa mnamo 2020-01-18.