Hubert Sumlin
Hubert Charles Sumlin (Novemba 16, 1931 - Desemba 4, 2011) alikuwa mpiga gitaa la muziki wa blues na mwimbaji kutoka jiji la Chicago huko Marekani [1]. Anajulikana zaidi kwa "noti za muziki zilizovunjika". Kama mwanachama wa bendi ya Howlin' Wolf [2] aliorodheshwa nambari 43 katika "Wapiga Gitaa 100 Wakubwa Zaidi wa Wakati Wote" ' Rolling Stone. [3]
Wasifu
[hariri | hariri chanzo]Sumlin alizaliwa huko Greenwood, Mississippi, na kukulia Hughes, Arkansas. [4] Alipatiwa gitaa lake la kwanza alipokuwa na umri wa miaka minane. [5] Akiwa mvulana mdogo , alikutana na Howlin Wolf baada ya kujiingiza kwenye tamasha lake bila kuwa na tiketi na hivyo kupata nafasi ya kukutana nae ana kwa ana.
Wolf alihama kutoka Memphis hadi Chicago mnamo 1953, ilhali mpiga gitaa wake wa muda mrefu Willie Johnson alichagua kutojiunga naye. Huko Chicago, Wolf alimuajiri mpiga gitaa Jody Williams, lakini mnamo 1954 alimwalika Sumlin kuhamia Chicago kucheza gitaa la pili katika bendi yake. Williams aliondoka kwenye bendi hiyo mnamo 1955, akimuacha Sumlin kama mpiga gitaa mkuu, nafasi ambayo aliishikilia kwa muda sana (isipokuwa kwa muda mfupi alipokuwa akicheza na Muddy Waters 1956). Kulingana na Sumlin, Howlin' Wolf alimtuma kwa mwalimu wa gitaa wa asili katika Conservatory ya Muziki ya Chicago ili kujifunza kinanda na mizani . [6] Sumlin alicheza kwenye albamu Howlin' Wolf (inayoitwa "rocking chair album", kwa kurejelea mchoro wake wa jalada), ambayo ilipewa jina la albamu ya tatu kubwa zaidi ya gitaa wakati wote na jarida la Mojo mnamo 2004.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Du Noyer, Paul (2003). The Illustrated Encyclopedia of Music. Fulham, London: Flame Tree Publishing. uk. 181. ISBN 1-904041-96-5.
- ↑ Kitts, Jeff; Tolinski, Brad (2002). Guitar World Presents the 100 Greatest Guitarists of All Time. Hal Leonard. p. 37.
- ↑ "43: Hubert Sumlin". The 100 Greatest Guitarists of All Time. Rolling Stone. Iliwekwa mnamo Desemba 18, 2015.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Komara, Edward, mhr. (2005). Sumlin, Hubert. Psychology Press. uk. 938. ISBN 9780415926997.
{{cite book}}
:|work=
ignored (help) - ↑ Gross, Jason. "Hubert Sumlin". Furious.com. Iliwekwa mnamo 2008-06-12.
- ↑ Segrest, James; Mark Hoffman (2004). Moanin' at Midnight: The Life and Times of Howlin' Wolf. New York: Thunder's Mouth Press. ku. 111–112. ISBN 1-56025-683-4.
Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Hubert Sumlin kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |