Howza

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Tshepo Howard Mosese (alizaliwa mnamo 19 Julai, mwaka1983) ni rapa kutoka nchini Afrika kusini, mtunzi wa nyimbo na mwigizaji.[1] Mosese alijihusisha na kwaya alipokuwa shule na mambo ya kitamaduni.[2] Alikuwa ni mwanachama wa kundi la Gunpowder. Baada ya kusajiiwa na lebo ya Faith Records mnamo mwaka 2007, alianza safari yake ya muziki wa solo na kuachia albamu yake iliyojulikana kwa jina la Cut to the Chase mnamo mwaka(2007).

Mosese pia alijiendeleza na maisha yake ya uigizaji na kushiriki maigizo kama Backstage, Scandal, 7de Laan, Big Up, All You Need is Love mnamo mwaka(2012).[3]

Maisha ya Awali[hariri | hariri chanzo]

Mnamo mwaka 2002 alijiunga na kikundi cha muziki wa wa hip hop cha Gunpowder ambacho kilikuwa, kwa muda huo chini ya lebo kama ya Kabelo Mabalane.[4] Mnamo mwaka 2007 kabelo, AKA Bouga Luv aliimpa ofa Howza ya kurekodi kama mwanamuziki wa solo chini ya faith records.

Maisha katika Uigizaji[hariri | hariri chanzo]

Howza amewahi kutokea katika igizo la Backstage la e.tv na kushiriki katika nafasi ya mhusika "Chase".[5] Pia amewahi kutokea katika igizo la Generations kama mhusika mkuu wa pili aliyejulikana kama "Adam" na pia kucheza kama "Lerumo Chabedi" kwenye South African soap opera Scandal!.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Tshepo Mosese | TVSA". www.tvsa.co.za. Iliwekwa mnamo 2022-04-24. 
  2. Door 6 Entertainment. "Howza | Musician, Actor and TV presenter". Door 6 Entertainment. Iliwekwa mnamo 2022-04-24. 
  3. Victor Brown (2021-01-26). "Howza Mosese – Biography, Age, Wife, Career & Net Worth » SANotify". SANotify (kwa en-US). Iliwekwa mnamo 2023-02-26. 
  4. "This will soon be the new home of the domain www.wowlive.co.za". web.archive.org. 2007-10-09. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-10-09. Iliwekwa mnamo 2022-04-24. 
  5. "The Times Planet Podcast » Blog Archive » Lesley Mofokeng chats to Howza". web.archive.org. 2007-09-28. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-09-28. Iliwekwa mnamo 2022-04-24.