Nenda kwa yaliyomo

Hospitali ya Nkoaranga

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Hospitali ya Nkoaranga inamilikiwa na Dayosisi ya Meru.

Hospitali hii ilianzishwa kama zahanati ndogo mnamo mwaka 1930. Hospitali hii inasimamia zahanati tano amabazo zipo ndani ya Dayosisi ya Meru. Zahanati hizi zinaweza kukubali idadi ya wateja kama 40 kwa uchunguzi wa muda mfupi. Zaidi ya wafanyakazi 80 hufanya Huduma za kiafya ndani ya Dayosisi ambayo idadi ya wakazi wake ni takribani 90,000.

Hospitali imekua sana katika kipindi cha miaka michache iliyopita chini ya uongozi wa sasa. Karibu miaka mitano iliyopita ilipendekezwa kuwa inapaswa kufungwa kwa sababu haikua na vigezo vya kuwa kama kituo cha afya, Lakini kwa msaada kutoka kwa vyanzo tofauti na usimamizi mzuri hospitali imevutia wagonjwa zaidi katika soko la afya la ushindani la eneo la Arusha na Mapambano ya huduma bora yameendelea. [1]

Mareeo[hariri | hariri chanzo]