Nenda kwa yaliyomo

Hifadhi ya Taifa Jebil

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Tunisia adm location map

Jebil ni mbuga ya kitaifa iliyopo nchini Tunisia iliyo ndani ya jangwa la Sahara, ikiwa na eneo la hekta 150,000. ni mbuga ya pili kwa ukubwa nchini Tunisia ikitanguliwa na hifadhi ya taifa ya Senghar-Jebbes. Ingawa ni kubwa pia ni mpya ikiwa imeteuliwa kuwa mbuga ya kitaifa mnamo mwaka 1994 (haikuwa rasmi tangu mwaka 1984). Kabla ya kutangazwa Senghar-Jebbes ilikuwa ndio mbuga pekee ya kitaifa ndani ya jangwa la Sahara.[1]

Mbuga ya wanyama ya Kitaifa ya Jebil ipo kilomita 80 kusini mwa Douz.Mimea inayopatikana katika mbuga hiyo ni vichaka vya mimea ya inayoota jangwani ambayo ndio inayopatikana kwa wingi, vichaka hivyo huwa vinatumika kama hifadhi ya swala, sungura pori na nyoka wanaopatikana katika mbuga hiyo. Mimea mingine inayopatikana ni maua aina yaRhanterium. Mbuga hiyo ina hifadhi kwa ajili ya watilii wanaofika hapo, walinzi wametapakaa karibu kila eneo la mbuga hiyo.Tafiti huwa zinafanyika katika mbuga hiyo kutokana sehemu hiyo kuwepo na idadi kadhaa ya vivutio vya sanaa ya kale ambazo hutumikana kujifunza kuhusu kipindi cha "Holecene" hadi kipindi cha vita ya pili ya Dunia.Mbuga hiyo imechukua nafasi kubwa ya "Grand Erg Oriental" .Sehemu ya magharibi kuna mawe makubwa yalioshikama na michanga na yanatokana na kumong'onyoka kwa mawe ya plutoniki

  1. "Defining a World Heritage in the Heart of the Libyan Desert". Agosti 2009.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)