Nenda kwa yaliyomo

Hifadhi ya Great Limpopo Transfrontier

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Hifadhi ya Greater Limpopo; kibichi cheusi ni hifadhi yenyewe, kibichi cheupe ni sehemu zinazotarajiwa ziunganishwe.

Hifadhi ya Great Limpopo Transfrontier au Great Limpopo Transfrontier Park ni hifadhi ya mazingira inayoandaliwa kwa shabaha ya kuunganisha maeneo yaliyohifadhiwa katika Afrika Kusini, Msumbiji na Zimbabwe. Nchi hizo tatu zilipatana mwaka 2002 kuunganisha hifadhi zao za Kruger, Gonarezhou na Limpopo, pamoja na Manjinji Pan Sanctuary na Malipati Safari Area, kwa jumla eneo la km² 35.000. Mipango inalenga kupanua eneo lake hadi kufikia km² 100,000.

Uzio kwenye mpaka kati ya Afrika Kusini na Msubiji umeshabomolewa na kuruhusu wanyama kutumia njia zao za zamani za uhamiaji ambazo zilizuiwa hapo awali kutokana na mipaka ya kisiasa.

Mnamo Oktoba 4, 2001 tembo 40 wa kwanza kati ya 1000 waliopangwa walihamishwa kutoka Hifadhi ya Kitaifa ya Kruger iliyojaa wanyama kwenda Hifadhi ya Taifa ya Limpopo iliyowahi kuathiriwa na vita ya wenyewe kwa wenyewe katika Msumbiji. Ilichukua miaka 2½ kumaliza uhamishaji.

Hifadhi itajumuisha maeneo yafuatayo[hariri | hariri chanzo]

 • Hifadhi kubwa ya Transfrontier ya Limpopo
  • Hifadhi ya kitaifa ya Kruger, karibu km² 18,989   (Ikiwa ni pamoja na Hifadhi za Wanyamapori za kibinafsi [1]. [2] )
  • Hifadhi ya Kitaifa ya Limpopo ( Msumbiji ) kama km² 10,000
  • Hifadhi ya Kitaifa ya Banhine ( Msumbiji ) karibu km² 7,000
  • Hifadhi ya Kitaifa ya Zinave ( Msumbiji ) karibu km² 6,000
  • Hifadhi ya Tembo ya Maputo ( Msumbiji ) karibu km² 700
  • Hifadhi ya Kitaifa ya Gonarezhou ( Zimbabwe ) karibu km² 5,053
  • Manjinji Pan Sanctuary (Zimbabwe)
  • Malipati Safari Area ( Zimbabwe )
  • Sengwe Safari Area ( Zimbabwe )

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

 1. "Hifadhi ya Wanyamapori Mjejane". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-04-19. Iliwekwa mnamo 2019-12-16.
 2. SANParks. "South African National Parks - SANParks - Official Website - Accommodation, Activities, Prices, Reservations".

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Hifadhi ya Great Limpopo Transfrontier kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.