Hermine Patricia Tomaïno Ndam Njoya

Hermine Patricia Tomaïno Ndam Njoya alizaliwa tarehe 26 Januari mnamo mwaka 1969 jijini Yaoundé, ni mwanasiasa, mjasiriamali, na mwandishi kutoka nchini Kamerun. Pia mwanachama wa Union démocratique du Cameroun (UDC) na ni mbunge katika Bunge la Taifa la Kamerun[1].
Hermine Patricia Tomaïno Ndam Njoya anaongoza kampuni ya kahawa na amekuwa rais wa Chama cha Wanawake wa Kamerun katika Sekta ya Kahawa (AFECC) tangu mwaka 2016. Hermine Patricia ni mjane wa Adamou Ndam Njoya, rais wa kitaifa wa UDC.
Elimu na Mafunzo
[hariri | hariri chanzo]Hermine Patricia Tomaino Ndam Njoya alizaliwa mjini Yaoundé mnamo 1969 na kukulia nchini Cameroon kati ya miji ya Yaoundé na Foumban. Baada ya kumaliza elimu ya msingi, alianza elimu ya sekondari mwaka 1980 katika Shule ya Upili ya Sultan-Njoya huko Foumban, na kumalizia kwa kupata shahada ya A4 baccalaureate mnamo 1987.
Baadaye, alijiunga na Chuo cha Sheria na Uchumi katika Chuo Kikuu cha Yaoundé, ambako alipata shahada ya kwanza ya sheria mwaka 1990 na shahada ya uzamili (Master's) katika Sheria ya Umma mnamo 1992.[2]
Mnamo 2001, alihudhuria Taasisi ya Kimataifa ya Watu Histadrut nchini Israel katika mpango maalumu kuhusu nafasi ya wanawake katika urejeaji wa mijini.
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Cameroun : Les femmes qui tiennent l'opposition - Hermine Patricia Ndam Njoya : L'adepte de la politique des résultats : Cameroun - Camer.be". camer.be (kwa Kifaransa). 2016-03-30. Iliwekwa mnamo 2017-09-09.
- ↑ "Députés de l'UDC". Union démocratique du Cameroun - UDC (kwa American English). 2016-05-29. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-09-09. Iliwekwa mnamo 2017-09-09.
| Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Hermine Patricia Tomaïno Ndam Njoya kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |