Henriette Ekwe Ebongo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Henriette Ekwe Ebo go

Henriette Ekwe Ebongo (25 Desemba , mwaka 1949)[1]ni mwandishi wa Kameruni, mchapishaji na mwanaharakati wa kisiasa. Alipewa Tuzo ya Kimataifa ya Wanawake wa Ujasiri mnamo mwaka 2011.[2][3]

Ebongo ni mtetezi wa uhuru wa vyombo vya habari, usawa wa kijinsia, haki za binadamu, na utawala bora. Alikuwa akihusika katika mapambano dhidi ya udikteta miaka ya 1980, na kampeni ya sasa dhidi ya ufisadi wa serikali, ubaguzi wa kijinsia na ukiukwaji wa haki za binadamu. Wakati huu amepata ukandamizaji, mateso, na kupelekwa katika mahakama ya jeshi.[2][4]

Yeye ndiye mchapishaji wa gazeti huru la kila wiki Babela na ni mwanzilishi wa tawi la Kamerun la Transparency International, kupambana na ufisadi shirika lisilo la kiserikali.[5]

Marejro[hariri | hariri chanzo]

People.svg Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Henriette Ekwe Ebongo kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.