Hege Storhaug
Hege Storhaug | |
---|---|
| |
Alizaliwa | 21 Mei 1962 |
Nchi | Norwei |
Kazi yake | Mwanaharakati na mwandishi wa vitabu |
Hege Storhaug (alizaliwa 21 Mei 1962) ni mwanaharakati wa kisiasa na mwandishi wa vitabu raia wa Norwei. Tangu miaka ya 1990 alijulikana kwa ukosoaji wake dhidi ya Uislamu na harakati zake za kupinga uhamiaji.[1][2] Kabla ya kujiingiza kwenye harakati za kupinga uhamiaji alifanya kazi kwa muda mfupi kama mwandishi wa habari. Anaongoza shirika dogo la kupinga uhamiaji liitwalo Human Rights Service akiwa na mshirika wake, na kushika nyadhifa ya mkurugenzi wa habari kwenye shirika hilo. Mwaka 2015 alichapisha kitabu cha Islam, den 11. landeplage chenye madai kuwa uislamu ni "hatari"[3][4][5] Wasomi na wachambuzi walifananua maoni yake kama chuki dhidi ya uislamu
Hapo awali, akiwa mchezaji wa mpira wa wavu, Storhaug pia alikuwa mkufunzi wa riadha aliyethibitishwa mwenye shahada ya kwanza kutoka chuo cha Norwegian School of Sport Sciences, na aliangazia matatizo ya kula kwa wanariadha wanawake. Aliwahi kucheza katika timu ya taifa ya wanawake ya mpira wa wavu ya Norwei, na alifundisha na kucheza katika timu ambazo ziliwahi kushinda mashindano ya kitaifa nchini Norwei.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Hege Storhaug", Store norske leksikon, 30 May 2012. (Norwegian)
- ↑ Haglund, Anniken (2008). "'For Women and Children!' The Family and Immigration Politics in Scandinavia". Katika Grillo, R. D. (mhr.). The Family in Question: Immigrant and Ethnic Minorities in Multicultural Europe. Amsterdam University Press. ku. 76–78. ISBN 9789053568699.
- ↑ "Produkten hittades inte". Bokus.com (kwa Kiswidi). Iliwekwa mnamo 2019-08-23.
- ↑ Rogne, Vebjørn (2016-02-26). "Storhaugs landeplage". BOK365.no (kwa Kinorwe cha Bokmal). Iliwekwa mnamo 2019-08-23.
- ↑ Storhaug, Hege. "Landeplagen på engelsk". Human Rights Service (kwa Kinorwe cha Bokmal). Iliwekwa mnamo 2019-08-23.
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Hege Storhaug kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |