Nenda kwa yaliyomo

Hassiba Ben Bouali

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Hassiba Ben Bouali[1] alizaliwa El-Asnam (sasa Chlef),[2] Algeria, katika familia ya kifalme.[3]

Wazazi wake walihamia Algiers mwaka 1947, ambapo alisoma katika shule ya upili ya Lycée Delacroix. Ali jiunga na Harakati za Skauti, na safari zake zilimfanya atambue hali ya watu wa Algeria chini ya utawala wa kikoloni. Hii ilimchochea kujiunga na Umoja wa Jumla wa Wanafunzi Waislamu wa Algeria (Union générale des étudiants musulmans algériens) mwaka 1954, akiwa na umri wa miaka 16. Alihusika katika harakati za kitaifa hadi kifo chake. Katika Vita vya Algiers vya 1957, yeye na wenzake watatu wakiwemo Ali Ammar (anayejulikana kama Ali La Pointe) waliuawa wakati majeshi ya Kifaransa yalipolipua maficho yao katika Casbah.

Ben Bouali aliigizwa katika filamu The Battle of Algiers na mwigizaji Fusia El Kader. Moja ya barabara kubwa zaidi huko Algiers na chuo kikuu cha Chlef vilipewa jina lake.

  1. "Hassiba, la femme d'exception ! | Youcef Elmeddah". web.archive.org. 2018-02-17. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-02-17. Iliwekwa mnamo 2024-09-28. {{cite web}}: no-break space character in |title= at position 32 (help)CS1 maint: bot: original URL status unknown (link)
  2. "Hassiba, la femme d'exception ! | Youcef Elmeddah". web.archive.org. 2018-02-17. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-02-17. Iliwekwa mnamo 2024-09-28. {{cite web}}: no-break space character in |title= at position 32 (help)CS1 maint: bot: original URL status unknown (link)
  3. "Hassiba, la femme d'exception ! | Youcef Elmeddah". web.archive.org. 2018-02-17. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-02-17. Iliwekwa mnamo 2024-09-28. {{cite web}}: no-break space character in |title= at position 32 (help)CS1 maint: bot: original URL status unknown (link)