Hamshahri
Hamshahri | |
---|---|
Jina la gazeti | Hamshahri |
Aina ya gazeti | *. Gazeti la kila siku *. Gazeti katika lugha ya Kiajemi |
Eneo la kuchapishwa | Iran |
Nchi | Iran |
Mwanzilishi | Gholamhossein Karbaschi |
Mchapishaji | Manispaa ya Tehran |
Makao Makuu ya kampuni | Tehran |
Nakala zinazosambazwa | 400,000 kila siku |
Tovuti | http://hamshahrionline.ir/ |
Hamshahri ni gazeti kuu la kitaifa la Iran katika lugha ya Kiajemi linalochapishwa na Manispaa ya Tehran, na lilianzishwa na Gholamhossein Karbaschi. Hili ndilo gazeti la kila siku, la kwanza la Iran linalochapishwa katika rangi zote mbalimbali. Lina kurasa 60 za matangazo na bei yake ni riali 1000 za Iran. Hivi sasa, gazeti hili lina usambazaji wake katika maeneo ya manispaa ya Tehran. Usambazaji wake wa kila ni nakala 400,000 kila siku, huu ni sawa na usambazaji wa magazeti makuu ya Marekani kama San Francisco Chronicle, Boston Globe na Chicago Tribune. [1]
Hamshahri na Uchaguzi wa Khatami
[hariri | hariri chanzo]Katika mwaka wa 1997 wa uchaguzi wa rais nchini Iran, gazeti la Hamshahri, lililoendeshwa wakati huo na Meya wa Tehran,Gholamhossein Karbaschi, lilishitakiwa na wahafidhina kuwa linaunga Khatami. Hii ilionekana kuwa haramu kwa sababu gazeti ambalo linapata ruzuku ya serikali haikukubalishwa kuchukua upande wowote katika uchaguzi. Suala hili ,hatimaye, lilisababisha Karbaschi kupelekwa kortini na kushtakiwa kwa kesi za kufuja mali na akahukumiwa kufungwa jela. Katika muhula wa pili wa Khatami, korti ikahukumu kuwa gazeti hilo linaweza kusambazwa ndani ya Tehran tu.
Shindano la Kimataifa la Uchoraji Katuni
[hariri | hariri chanzo]Mnamo 6 Februari 2006, Farid Mortazavi, mhariri wa picha wa Hamshahri, alitangaza Shindano la Kimataifa la Uchoraji Katuni Za Holocaust. Shindano hili lilikuwa ili kukemea lililoita "unafiki wa nchi za Magharibi katika uhuru wa kujieleza" huku Hamshahri likidai kuwa nchi za Magharibi hazifai kujadili mada fulani kuhusu Uyahudi kama vile , vifo vya Holocaust. Shindano hili liliisha tarehe 1 Novemba 2006 huku Abdellah Derkaoui, mchoraji katuni wa Moroko, akishinda nafasi ya kwanza.
Kupigwa Marufuku
[hariri | hariri chanzo]Gazeti hili liliachishwa kuchapishwa mnamo 23 - 24 Novemba 2009 baada ya kuchapisha picha ya hekalu ya dini iliyopigwa marufuku ya Bahá'í.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- "Iran's liberal press tiptoes between "red lines"". 11 Juni 2007. .
- "Iran Shuts Newspaper For Publishing Baha'i Temple Photo"
- Hafezi, Parisa; Jaseb, Hossein; Mostafavi, Ramin (24 Novemba 2009). Ban on Iran paper over Baha'i photo lifted. Reuters.
- In Iran, ban on popular Hamshahri daily lifted. Archived 23 Septemba 2012 at the Wayback Machine.Press TV. 24 Novemba 2009
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Hamshahri.org tovuti ya hamshahri (Lugha ya Kiajemi)
- Hamshahri.org tovuti ya hamshahri (Lugha ya Kiajemi)
- Hamshahri.com tovuti ya hamshahri (Lugha ya Kiajemi na Kiingereza)
- tovuti ya hamshahree Archived 1 Septemba 2011 at the Wayback Machine. (Lugha ya Kiajemi)
- Katuni za Holocaust Archived 4 Januari 2016 at the Wayback Machine. - katuni za Hamshahri, na maoni ya irregulartimes.com
- Copyright Infringement by Hamshahri (Lugha ya Kiajemi na Kiingereza)
- ↑ Toleo la gazeti hili linaweza kupatikana katika tovuti yake ya hamshahrionline.ir