Nenda kwa yaliyomo

Gulf Daily News

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Gulf Daily News
Jina la gazeti Gulf Daily News
Aina ya gazeti *. Gazeti la kila siku
*. Gazeti la lugha ya Kiingereza
Lilianzishwa Machi 1978
Eneo la kuchapishwa Bahrain
Nchi Bahrain
Mwanzilishi Kundi la Al Hilal
Mhariri George Williams
Mmiliki Kundi la Al Hilal
Mchapishaji Kundi la Al Hilal
Makao Makuu ya kampuni Manama
Nakala zinazosambazwa 10,000 zilizolipiwa kila siku
Tovuti http://www.gulf-daily-news.com/

Gulf Daily News (Swahili:Habari za Kila Siku za Ghuba) ni gazeti lililichapishwa kwa lugha ya Kiingereza katika Ufalme wa Bahrain na Kundi la Al Hilal. Linasambazwa katika mitaa ya Bahrain. Inamilikiwa na Kundi la Al Hilal ambalo huchapisha magazeti mengine 13 kama lile la Kiarabu la Akhbar Al Khaleej. Jarida hili, ambalo ni mojawapo ya magazeti ya kila siku nchini Bahrain, linajiita "Sauti ya Bahrain". Jina lake hufupishwa kuwa GDN.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

GDN lilikuwa gazeti la kwanza la lugha ya Kiingereza la kuchapishwa nchini Bahrain. Lilianzishwa Machi 1978, na Kundi la Al Hilal. Mpaka gazeti la Bahrain Tribune lilipoanza kuchapishwa, gazeti hili lilikuwa gazeti pekee la Kiingereza nchini Bahrain.

Jarida hili liliundwa kwa lengo la kutoa habari kwa wakazi wa Bahrain wanaozungumza Kiingereza, wakijumuisha Waingereza, Wamarekani,Wafilipino, Wahindi na Wapakistani. Wafanyakazi wa GDN ni mchanganyiko wa Waingereza, Wamarekani, Wafilipino, Wahindi na Wapakistani.

Hapo awali, Gulf Daily News lilikuwa likiunga serikali lakini baada ya mageuzi ya kisiasa ya 2001, hivi sasa,linaajiri Waislamu na ,vilevile,watu wenye misimamo mingine kama wafanyikazi. Gazeti hili lina waandishi kadhaa ambao huandika makala mbalimbali kuhusu masuala ya Bahrain kama Les Horton, Amira Al Hussaini, Ali Al Saeed na Tariq Khonji.

Waandishi

[hariri | hariri chanzo]

Hivi sasa, GDN limeajiri baadhi ya waandishi bora na maarufu wa eneo la Ghuba ya Kiajemi. Hawa ni: Mbahraini Mohammed Al A'ali, Mwingereza Rebecca Torr, Mbahraini Sara Sami, Mwingereza Sara Horton, Mhindi Begena George, Geoffrey Bew(Scotland), Mhindi Mandeep Singh, Mhindi Alistair Baptista, Mfilipino Patrick Salomon.

Waandishi Mwamerika Richard Moore na Mhindi Vinitha Vishwanath Waliaga dunia katika mwaka wa 2006 na hivi majuzi zaidi, Mbahraini Mohammed Aslam

GDN la leo

[hariri | hariri chanzo]

Gulf Daily News ndilo gazeti la kila siku maarufu kabisa nchini Bahrain. Gazeti sasa linamilikiwa na Kundi la Al Hilal. Jarida hili lina makao nchini Bahrain huku ofisi zake za uhariri zikipatikana Isa Town na ofisi za kibiashara zinapatikana katika barabara ya Exhibition Road.

Jarida hili lina usambazaji wa nakala 10,000 zilizolipiwa. Lina kurasa takriban 40. Huchapishwa katika rangi nyeusi na nyeupe na kurasa zingine katika rangi zingine. Habari zake huwa kimsingi kuhusu Bahrain, isiasa na jamii lakini huhusisha habari za biashara ya kimataifa na habari za kijamii zitakaovutia wasomaji.

Sehemu kuu

[hariri | hariri chanzo]

Gazeti hili Hupangwa katika sehemu nne:

1.Habari
Huhusisha za kimataifa, kitaifa, biashara, michezo na hali ya anga.
2. Maoni
Huhusisha makala ya mhariri, maoni ya mhariri na nyaraka zilizotumiwa kwa mhariri.
3. Vipengele
Huhusisha ratiba za sinema, matukio nchini, michezo midogo, katuni na ratiba za stesheni za televisheni.
4. Matangazo


Jarida hili lina ukubwa wa 36 cm x 26 cm kwa kila ukurasa na upana wa 3.45 cm kwa kila makala kwa ukurasa. Huchapishwa kwa kutumia Web Offset na huchapishwa kwa kutumia skrini ya 100 lpi (Nyeusi na nyeupe).

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]