Godfrey Semwaiko

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Godfrey Steven Semwaiko (alizaliwa 4 Oktoba 1975) ni mchongaji wa sanamu na pia mchoraji kutokea shule ya uchongaji ya Bagamoyo, Tanzania. Pia ni mmoja wa waanzilishi wa Chama cha Wasanii Tanzania. [1]

Elimu[hariri | hariri chanzo]

Godfrey alijiunga na shule ya msingi Mkoani iliyopo Kibaha. [2] Alisoma shule ya sekondari Kibaha na kufanikiwa kutunukiwa cheti cha elimu hiyo ya sekondari katika ngazi ya kidato cha kwanza hadi cha nne mwaka 1992. Aliweza kuendelea na masomo yake ya elimu ya sekondari, kidato cha tano na cha sita katika shule hiyo hiyo ya sekondari ya Kibaha na mnamo mwaka 1995 alitunukiwa cheti cha kuhitimu. Mwaka 1997, Godfrey aliweza kujiunga na mafunzo katika mradi wa Uchongaji wa Sanamu, Sculpture project Bagamoyo, Tanzania - art education chini ya Stanislaw Lux[3], nakuibuka kidedea kwa kutunukiwa cheti cha mwaka mmoja cha Usanifu na Sanaa mwaka 1998. Mwaka mmoja baadae, Godfrey aliweza kujiunga na masomo ya Sanaa nchini Uswidi[4] ambapo alihitimu mwaka 2001. [5]Mwaka 2013 alijiunga na Taasisi ya Kiteknolojia ya Dar es salaam, Dar es Salaam Institute of Technology (DIT)[6] kwa miaka mitatu na kuhitimu pia kutunukiwa cheti cha mwanafunzi bora katika kozi ya Multimedia and Film Technology. Katika kujiendeleza kielimu, Godfrey alijiunga na chuo kikuu cha Asia (Asia University)[7], nchini Taiwan na kuhitimu shahada ya uzamili katika "Digital Media Design"[8] mwaka 2022. Katika kujiendeleza kitaaluma, mwaka 2023, Godfrey alihitimu kozi ya mwaka mmoja na kutunukiwa cheti cha ualimu katika programu ya TEACH-NOW®[9] ambayo hufundisha kozi ya kiwango cha wahitimu inayohitajika kwa uthibitisho mbadala wa kufundisha toka chuo kikuu cha Moreland[10] nchini USA.

Kazi[hariri | hariri chanzo]

Godfrey ni msanii anayeshughulika na uchoraji, uchongaji wa sanamu na sanaa za kidijitali ikiwemo vitabu ingiliani, ukaragushi, michoro rembo pamoja na utengenezaji wa filamu [11]

Godfrey pia anapenda kufundisha kwa kujumuisha sanaa za jadi za ufundi kama uchoraji, uchongaji nk katika sanaa ya kidijitali kwa kutumia utafiti na matumizi ya akili bandia.[12] Kwa uwasilishaji wake katika mkutano wa kimataifa, International Conference on Studies in Engineering, Science, and Technology (ICSEST) uliofanyika Octoba 20-23, 2023 imjini Antalya, Uturuki. Godfrey alipokea tuzo ya "Tafiti Bora," ambayo ilitolewa kwa wasilisho ambalo lilipitiwa na kutawaliwa na wanakamati kulingana na uhalisi, mbinu, na matokeo ya utafiti[13].

Godfrey amewahi kufanya kazi katika taasisi mbalimbali nchini tanzania na nje ya Tanzania, kwa mikataba ya muda mfupi na mrefu, ikiwemo Independent Television Tanzania (ITV)[14] mwaka 2001. Mwaka 2005 - 2006 aliajiriwa nchini Uingereza kwenye mradi wa utunzaji mazingira kwa ajili ya kutayarisha na kuchora michoro ya kitabu cha kufundishia mbinu mbalimbali za kutunza mazingira kwa nchi za Afrika, Pan- African Conservation Education (PACE).[15] Mwaka 2007 - 2012 alianzisha na kuiongoza kampuni yake binafsi ya sanaa na burudani yenye kutayarisha michoro, makala za video, na kurekodi muziki, ikiwa na studio ya kurekodi, iitwayo Usanii Production LTD.[16] ambapo baadae ilimuajiri mtayarishaji kutoka nchini Uswidi, Fundi Samweli na aliyekuwa mkewe Sara Lundstrom a.k. Saraha. Baadhi ya kazi zilizozalishwa na Usanii Production Ltd, ni pamoja na Fei[17], wa Farid Kubanga[18], a.k.a Fid Q, Sweety Sixteen[19] (Nako 2 Nako feat. Fundi Samweli), My Dear[20], Jambazi[21], Tanesco[22] zote zilizoimbwa na kushirikishwa mwanamuziki Saraha[23]Nikumbatie[24] wa Joh Makini[25] ft Fundi Samweli. Aifola[26] wa Linex[27] Feat. Fundi Samweli.

Uzoefu[hariri | hariri chanzo]

Godfrey ana uzoefu wa muda mrefu katika kazi za uchoraji vitabuni, uhariri na utayarishaji wa makala za video, vipindi vya Televisheni, Filamu za animation, pia uchoraji wa kidijiti (Digital Art). Baadhi ya kazi alizozizalisha katika utayarishaji wa makala ni pamoja na makala ya kuadhimisha miaka 40 ya Shirika la Elimu Kibaha[28], Mafanikio ya Mfuko wa Utamaduni Tanzania (Tanzania Education Authority - TEA[29]), makala maalumu inayomhusu Dr. David Urkevist[30], Kuandaa vipindi vya Televisheni kuhusu programu za Plan International Tanzania[31] vya kupambana na haki za watoto wa kike na mimba za utotoni[32]. Godfrey ameshiriki katika utungaji na utayarishaji wa filamu fupi ya animation iitwayo Toto's Journey

Pia Godfrey ameongoza na kusimamia utayarishaji na urukaji wa vipindi vya "Safari ya Dodoma", kwenye Televisheni ya TBC[33]

Uchoraji na Usanifu wa Vitabu uliofanywa na Godfrey Semwaiko
Jina la Kitabu Mchapaji/ Mtayarishaji Mwandishi Mwaka
Mtoto Katika Nyumba ya Chatu[34] Vitabu Vya Kibaha, Tanzania Josephat Seng’enge 1995
Zimwi na Chanzo Kipya cha Maji WaterAid Tanzania Project[35] Tanya Zebroff 1998
CBP catalogue 1999 – 2000 Tanzania Children's Book Project (CBP) CBP[36] 1999
Amabhuku (illustrations from Africa)[37] La Joie par les livres 1999
Leo ni Siku Gani[38] E & D Ltd[39] Alice K Rugu 2000
Mtawa na Binti Mfalme[40] Ruvu Publishers Co. Ltd[41] W.E Mkufya[42] 1998, 2002
Mvua Yenye Balaa[43] Tanzania Educational Publishers[44], CBP Johansen N Machume 2002
Majigambo ya Wadudu[45] Tanzania Educational Publishers[44], CBP Johansen N Machume 2002
Mapambano[46] Tanzania Educational Publishers[44], CBP Johansen N Machume 2002
Mzee Alfabeti[47] Tanzania Educational Publishers[44], CBP Johansen N Machume 2002
Kabo and The Rain God Heinemann Educational; Oxford, UK Anthony Umelo 2002
Femina Magazine

Kuishi Kwa Matumaini na Virusi Vya UKIMWI UKIMWI Katika Jamii Yetu VVU na UKIMWI Huathiri Watoto Pia VVU, UKIMWI na Tiba

Femina-Hip, Tanzania Archived 13 Februari 2024 at the Wayback Machine. 2003

2004 2006

Hadithi isiyo na mwisho, Fisi na Kucha za Simba, Watoto na Zimwi, Kaona Njigi kadhani Njege, Ua la Zalizali, Nora na Matunda ya Ajabu, Popo Ndege na Panya, Karibu Social Studies (Teachers Guide, Grades 1&2), Karibu Social Studies Grade 1 & 2, Haramu, Spared, Nataka kuwa tajiri, Msako, Diwani ya Ustaadhi Nyamaume, Guberi Mfawidhi na Rusa, Diwani ya Jinamizi, Elimu Jamii na Chemsha Bongo kwa Mashairi, Masimulizi ya Alfu Lela U Lela 1-4 (Cover designs), Mafunzo ya Uzazi wa Mpango (Cover Design), Wasifu wa Siti Biti Saad. Mkuki na Nyota Publishers waandishi mbalimbali 2002-2008
PRESIDENTKANDIDATEN Vitabu Vya Kibaha Munga Tehenani 2005
Africa Our Home PACE, TUSK-UK Sasha Norris 2006 - 2019
Rehema has a Cat, Nataka Keki yangu, Marimba ya Majaliwa, Elimu ya Mazingira – NISHATI (WWF Tanzania Environmental Education Programme), Elimu ya Mazingira – Bahari (WWF Tanzania Environmental Education Programme) E&D Vision Publishers Waandishi mbalimbali 2000-2007
Aisha, Mussa, Zawadi (Usanifu kwa toleo la Kiswahili) Tanzania –Switzerland Cooperation Elisabeth Kaestli 2011

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. https://www.saahiihii.com/storyPage.php?lang=SWT&page=ABOUT&section=ART_ENTERT&story=1&businessNo=1308&action=card
  2. https://www.thecitizen.co.tz/magazine/soundliving/PROFILE---Telling-stories-through-art/1843780-3385814-oguapdz/index.html
  3. Om mig :: Stanislawlux-com (sv). stanislawlux-com.webnode.se (2023-04-13). Iliwekwa mnamo 2024-02-13.
  4. Hjo Konstskola - konstnärligt projektår - folkhogskola.nu (sv). www.folkhogskola.nu. Iliwekwa mnamo 2024-02-13.
  5. https://www.saahiihii.com/storyPage.php?lang=SWT&page=ABOUT&section=ART_ENTERT&story=1&businessNo=1308&action=card
  6. Dar es Salaam Institute of Technology. www.dit.ac.tz. Iliwekwa mnamo 2024-02-13.
  7. Asia University, Taiwan 歡迎光臨亞洲大學全球資訊網. web.asia.edu.tw. Iliwekwa mnamo 2024-02-13.
  8. Dept. of Digital Media Design, Asia University (en). Dept. of Digital Media Design, Asia University. Iliwekwa mnamo 2024-02-13.
  9. Online Teaching Certification (en). Moreland University (2023-12-19). Iliwekwa mnamo 2024-02-13.
  10. Home (en). Moreland University (2023-12-19). Iliwekwa mnamo 2024-02-13.
  11. https://www.imdb.com/name/nm2379694/bio?ref_=nm_ov_bio_sm
  12. ISTES-International Society for Technology, Education and Science. Proceedings of International Conference on Studies in Engineering, Science, and Technology 2023 (en). www.istes.org. Iliwekwa mnamo 2024-02-13. https://www.istes.org/proceedings-of-international-conference-on-studies-in-engineering-science-and-technology-2023-56-b.html
  13. Best Paper Award | International Conference on Studies in Engineering, Science, and Technology. www.2023.icsest.net. Iliwekwa mnamo 2024-02-13.
  14. ITV - Independent Television (en). ITV - Independent Television. Iliwekwa mnamo 2024-02-13.
  15. PACE-WWW-Admin. PACE (en-GB). PACE - Pan African Conservation Education. Iliwekwa mnamo 2024-02-13.
  16. About. www.saahiihii.com. Iliwekwa mnamo 2024-02-13.
  17. Fareed Kubanda a.k.a Fid Q - FEI (in sw-TZ), retrieved 2024-02-13 
  18. "Fid Q", Wikipedia, kamusi elezo huru (in Swahili), 2024-01-13, retrieved 2024-02-13 
  19. Sweety Sixteen (feat. Fundi Samweli) (in sw-TZ), retrieved 2024-02-13 
  20. AKIL THE BRAIN FT BIGJAHMAN & SARAHA - My Dear (Video Music Official) (in sw-TZ), retrieved 2024-02-13 
  21. SaRaha Jambazi [Official Video] 2012 (in sw-TZ), retrieved 2024-02-13 
  22. SaRaha Tanesco (in sw-TZ), retrieved 2024-02-13 
  23. "Saraha", Wikipedia (in Swedish), 2024-02-11, retrieved 2024-02-13 
  24. JohMakini ft Fundi Samweli - Nikumbatie (in sw-TZ), retrieved 2024-02-13 
  25. "Joh Makini", Wikipedia (in English), 2024-01-19, retrieved 2024-02-13 
  26. Linex Feat. Fundi Samweli - Aifola (in sw-TZ), retrieved 2024-02-13 
  27. Linexsundaymjeda - YouTube. www.youtube.com. Iliwekwa mnamo 2024-02-13.
  28. SHIRIKA LA ELIMU KIBAHA_ MIAKA 40 (in sw-TZ), retrieved 2024-02-13 
  29. TANZANIA EDUCATION AUTHORITY TEA (in sw-TZ), retrieved 2024-02-13 
  30. THE LAST INTERVIEW WITH THE LATE DR DAVID URKEVIST (in sw-TZ), retrieved 2024-02-13 
  31. Plan International - Tanzania (en-GB). Plan International Tanzania. Iliwekwa mnamo 2024-02-13.
  32. MWANZA SCHOOL GIRLS DEBATE ON EARLY PREGNANCY (in sw-TZ), retrieved 2024-02-13 
  33. "Tanzania Broadcasting Corporation", Wikipedia (in English), 2024-01-19, retrieved 2024-02-13 
  34. Mtoto katika nyumba ya chatu | WorldCat.org (en). search.worldcat.org. Iliwekwa mnamo 2024-02-13.
  35. Tanzania | WaterAid UK (en). www.wateraid.org. Iliwekwa mnamo 2024-02-13.
  36. The Children's Book Project (en). The Communication Initiative Network. Iliwekwa mnamo 2024-02-13.
  37. "Amabhuku", Wikipedia (in Italian), 2019-04-29, retrieved 2024-02-13 
  38. Maktaba.org - Free Education | Leo ni Siku Gani?. www.maktaba.org. Iliwekwa mnamo 2024-02-13.
  39. END Vision Publishers Limited Company. www.edvisionpublishing.co.tz. Iliwekwa mnamo 2024-02-13.
  40. Mwanga, Abel K.; Mkufya, W. E. (1998). Mtawa na binti mfalme (in Swahili). Ruvu Publishers. ISBN 978-9976-965-18-6. 
  41. 😀😡😇 Ruvu Publishers Ltd, Companies & Businesses, Tanzania, ...022 211 5. www.africanadvice.com. Iliwekwa mnamo 2024-02-13.
  42. W. E. Mkufya - Google Search. www.google.com. Iliwekwa mnamo 2024-02-13.
  43. Mvua yenye balaa | WorldCat.org (en). search.worldcat.org. Iliwekwa mnamo 2024-02-13.
  44. 44.0 44.1 44.2 44.3 TANZANIA EDUCATIONAL PUBLISHERS LTD Store Ecommerce Website (en). www.tepu.co.tz. Iliwekwa mnamo 2024-02-13.
  45. Majigambo ya wadudu | WorldCat.org (en). search.worldcat.org. Iliwekwa mnamo 2024-02-13.
  46. Mapambano | WorldCat.org (en). search.worldcat.org. Iliwekwa mnamo 2024-02-13.
  47. Mzee alfabeti | WorldCat.org (en). search.worldcat.org. Iliwekwa mnamo 2024-02-13.
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Godfrey Semwaiko kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.