Nenda kwa yaliyomo

Godfrey Calvin Magila

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Godfrey Calvin Magila (alizaliwa mkoa wa Mbeya, 28 Februari 1992 [1]) ni mhasibu kwa taaluma na ni Mwana TEHAMA mwanzilishi wa Kampuni ya Magilatech ambayo inajihusisha na kutengeneza mifumo mbalimbali ya Kompytuta. Magila ni mmoja kati ya vijana walioanzisha kampuni wakiwa na umri mdogo ndani ya Tanzania na kuweza kufanikiwa.

Maisha Yake

[hariri | hariri chanzo]

Akiwa na umri wa miaka 5 Godfrey alipata pigo la kufiwa na mama yake mzazi ingawa hakuwahi kulelewa na baba mzazi kwani alifariki Godfrey akiwa na umri wa miezi mitatu tu. Akalelewa na ndugu zake kuanzia mwaka 1998 ambapo mwaka 2010 na mwaka 2011 ukawa mwaka mwingine wenye pigo kwake kwa kupoteza walezi wake wote wawili [2].

Elimu Yake

[hariri | hariri chanzo]

Alisoma shule ya Mbezi Beach High School iliyopo jijini Dar es salaam. Mwaka 2010 alijiunga na chuo kikuu cha IFM kusomea kozi ya uhasibu.

Kupitia kampuni yake ya Magilatech, Godfrey amekuwa akitengeneza mifumo katika kampuni na taasisi ndani na nje ya Tanzania ambapo pia amefungua kampuni Dubai[3] na kuajiri wafanyakazi wengi kutoka nchi mbalimbali. Serikali ya Tanzania inamtambua na inajivunia kama kijana mwenye mchango mkubwa. “Kuna vijana wametoka wazuri katika hii mifumo yetu chukua mfano kuna kijana anaitwa Magila kutoka Magilatech yeye ameanza na Costech (Atamizi ya Tume ya Science na Technolojia) yuko DRC anatengeneza mifumo ni kijana wa kitanzania” - Rais Samia Suluhu Hassan[4]

Tuzo na Teuzi

[hariri | hariri chanzo]
  1. Start-up World Africa - Top Ten Finalist (2012)
  2. Innovation Fund  award  for best app (2014)
  3. Global Recognition  Of Excellence - ITU Hungary (2015)
  4. 30 Under 30 By Forbes (2017)
  5. Innovator of the year - All Africa Bussiness Learders ( Awards AABLA ) - East Africa (2017)
  6. Top100 midsized Companies By KPMG, The Citizen (2018)
  1. https://www.startupgrind.com/events/details/startup-grind-dar-es-salaam-presents-godfrey-magila-magilatech-company-ltd/
  2. https://www.thecitizen.co.tz/tanzania/magazines/success/how-a-passionate-gamer-built-a-tech-company-3799654
  3. https://millardayo.com/magiladubai/
  4. https://millardayo.com/rais-samia-atambua-mchango-mkubwa-wa-magila-tech-aeleza-mipango-ya-serikali-katika-hili/

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
  1. https://wsa-global.org/person/3535/
  2. https://talkafricana.com/forbes-africa-list-of-30-under-30-most-promising-young-african-entrepreneurs-2017/
  3. https://www.thecitizen.co.tz/tanzania/magazines/success/tanzania-s-top-tech-players-share-pathways-to-success-4098672
  4. https://www.bellanaija.com/2017/06/forbes-africa-30-under-30-2017-list-see-young-entrepreneurs-doing-great-things/