Gladness Deogratias
| Gladness Deogratias | |
| Nchi | Tanzania |
|---|---|
| Majina mengine | Gladness |
| Kazi yake | Amesomea Masuala ya Biashara |
| Mwajiri | Benki ya NMB |
| Cheo | Mkuu wa Idara ya Fedha za Kigeni katika Benki ya NMB |
| Dini | Mkristo |
| Ndoa | Ameolewa |
| Watoto | 3 |
| Mahusiano | Ni mke wa watoto watatu |
Gladness Deogratias ni Mkuu wa Idara ya fedha za kigeni katika Benki ya NMB nchini Tanzania. [1]
Elimu
[hariri | hariri chanzo]Gladness alipata elimu ya shule ya msingi mkoa wa Dar es Salaam katika Shule ya Msingi Chang’ombe na kuhitimu darasa la saba mwaka 1996. Baadaye alijiunga na Shule ya Sekondari Kifungilo na kuhitimu kidato cha nne mwaka 2000. Baada ya kuhitimu elimu ya sekondari alifanikiwa kupata nafasi ya ufadhili wa masomo kupitia International School of Tanganyika na kujifunza masomo ya Saikolojia. Mwaka 2006 Alihitimu shahada ya sanaa katika usimamizi wa masuala ya fedha chuo kikuu cha Nottimghan huko Nottimghan, Uingereza. Alihitimu Shahada ya pili ya Usimamizi wa biashara mwaka 2014 katika chuo kikuu cha Oxford Brookes huko Oxford, Uingereza.
Taaluma
[hariri | hariri chanzo]Baada ya kuhitimu chuo kikuu mwaka 2006 aliomba kufanya kazi katika benki ya LEHAM International European Bank ambapo alidumu kwa muda wa miaka miwili kisha kuamua kurudi nyumbani kwao Tanzania baada ya kutokea kwa mtikisiko wa Dunia kiuchumi uliopelekea kufungwa kwa benki hiyo. Baada ya kurejea Tanzania, Gladness alianza kufanya kazi katika benki ya ABC kisha kuhamia benki ya NMB akifanya kazi kama Mkuu wa Biashara na baadae kupandishwa cheo na kuwa Mkuu wa Idara ya Fedha za Kigeni katika Benki hiyo ya NMB, Cheo alichodumu nacho hadi sasa. Akiwa mfanyakazi wa NMB Gladness amekuwa mstari wa mbele katika kuleta chachu ya usawa wa kijinsia kati ya wanawake na wanaume katika benki hiyo.
Familia
[hariri | hariri chanzo]Gladness Deogratias ameolewa na kujaliwa kupata watoto wawili ambao ni wa kiume Quinlan na Quintrell.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Napambana-kuwainua-wanawake-nmb-Gladness". Mtanzania. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-10-24. Iliwekwa mnamo 7 Machi 2019.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
| Makala hii kuhusu wasifu wa Mtanzania bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |