Giordano Bruno

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Giordano Bruno

Giordano Bruno (Nola, 1548 - [[Roma], 17 Februari 1600) alikuwa kasisi, mtawa wa shirika la Wadominiko, mwanafalsafa na mshairi nchini Italia.

Anakumbukwa katika falsafa hasa kwa sababu ya mafundisho yake kuwa ulimwengu hauna mwisho wala mipaka.

Kwa ajili hiyo alihukumiwa na mahakama ya Papa adhabu ya kifo na kuchomwa moto kama mzushi na mchawi.

Mwaka 2000 kamati ya Vatikano ilitangaza kwamba hukumu ile ilikuwa na kosa.


Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.