Gilberto Gil

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Gilberto Gil, waziri wa utamaduni wa Brazil

Gilberto Passos Gil Moreira (alizaliwa 26 Juni 1942) ni mwanamuziki, mwimbaji, mpiga gitaa, na mwanaharakati toka nchini Brazili. Gil alikuwa Waziri wa Utamaduni wa nchi hiyo toka mwaka 2003 to 2008 katika serikali ya Rais [[Luiz Inácio Lula da Silva]].

Gil alianza safari yake ndefu ya muziki akipiga muziki aina ya Bossa Nova kisha baadaye akaanza kuandika nyimbo za kuchochea mwamko na ufahamu wa kisiasa na kijamii.

Mwaka 1969, Gil na mwanamuziki mwenzake, Caetano Veloso walikamatwa na askari wa serikali ya kijeshi ya Brazili kwa tuhuma za kujihusisha na harakati dhidi ya serikali. Walipoachiliwa, wote wawili walikimbilia uhamishoni London, Uingereza.

Akiwa Uingereza, Gil alianza kutumbuiza na makundi ya muziki nchini humo kama vile Yes, Pink Floyd, na Incredible String Band. Mwaka 1970 alitembelea Marekani ambapo alirekodi santuri aliyoimba kwa Kiingereza. Akishirikiana na Jimmy Cliff alirekodi wimbo wa Bob Marley wa "No Woman, No Cry" mwaka 1980. Wimbo huu ulipata umaarufu mkubwa na ulifanikiwa kuifanya Rege kupendwa na kukubalika nchini Brazili.

Pamoja na kuwa waziri, Gil bado aliuwa akitumbuiza mwisho wa wiki na pia alirekodi nyimbo kadhaa akiwa waziri kama vile Rebento, Refavela, Refzenda, na Oslodum. Nyimbo hizi amezitoa chini ya mfumo mpya wa hatimiliki huria, Creative Commons.

Mei 2005, Mfalme wa Uswidi alimkabidhi Gil tuzo ya muziki ya "Polar Music Prize." Septemba 2005 alipewa tuzo ya "Légion d'honneur" toka serikali ya Ufaransa

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu: