Nenda kwa yaliyomo

Gianni Garko

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Graziella Granata na Gianni Garko wakiwa Don Camillo Moscow

Gianni Garko (amezaliwa kwa jina la Giovanni Garcovich mnamo mwaka 1935, mara nyingi jina lake hufupishwa kama John Garko) ni mwigizaji wa filamu kutoka nchini Yugoslavia, aliyepatia umaarufu katika western za kiitalia, hasa alivyoigiza kama Sartana, katika filamu yake ya kwanza iliyokuwa inaitwa If You Meet Sartana Pray for Your Death.

Garko pia alicheza katika filamu nyingine mbili za spaghetti western, ikiwemo ile ya Holy Ghost na Django. Garko alianza shughuli za uigizaji katika miaka ya 1958 hivi. Alicheza filamu ya kwanza mnamo mwaka 1967 kama Sartana, katika filamu ya Blood at Sundown.

Garko alipokelewa na George Hilton katika filamu ya I Am Sartana na Trade Your Guns for a Coffin. Garko pia ameonekana katika mfululizo wa filamu za kisayansi maarufu kama Space 1999.