Muungano wa Kijerumani
Muungano wa Kijerumani ( Kijerumani : Deutsche Wiedervereinigung , Kiing. German Reunification) ulikuwa mchakato wa kuunganisha sehemu za Ujeruamni zilizowahi kutenganishwa. Muungano huo ulitokea kwenye mwaka 1990 wakati majimbo ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Ujerumani (Ujerumani Mashariki) yalijiunga na Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani (Ujerumani Magharibi).
Baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia, Ujerumani iligawanywa na washindi kwa kanda nne vilivyosimamiwa na Marekani, Urusi, Uingereza na Ufaransa.
1949 Wajerumani walianza tena kujitawala katika nchi mbili. Kanda za Marekani, Uingereza na Ufaransa ziliungana kwa jina la Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani liliofuata siasa ya demokrasia ya vyama vingi na uchumi wa kibepari. Kanda la Kirusi lilikuwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kijerumani lililofuata siasa ya utawala wa chama cha kikomunisti na uchumi wa kijamaa.
Hadi mwaka 1960 uchumi wa magharibi umepita ule wa mashariki. Hali ya maisha katika magharibi ilianza kuwa bora na pamoja na udikteta wa kisiasa wa Wakomunisti wananchi wengi wa mashariki walivuka mpaka wakahamia magharibi. Kwa hivyo serikali ya mashariki ilianza kujenga fensi kwenye mpaka na kwenye Agosti 1961 ilijenga ukuta wa Berlin uliozuia watu wa mashariki wasiweze tena kufika magharibi.
Hadi mwaka 1989 hali ya kiuchumi katika mashariki ilizidi kubaki nyuma ya magharibi, na kwa jumla uchumi ulikuwa matatani. Wakati ule kiongozi wa Umoja wa Kisoveti Mikhail Gorbachev alianza kulegeza ukali wa utawala wa kikomunisti[1] . Watu wengi kwenye mashariki hawakuwa tena tayari kunyamaza na idadi ya wakimbizi wa kwenda magharibi iliongezeka kwa ghafla wakipita nchi jirani za kikomunisti kama Chekoslovakia na Hungaria ambako watawala hawakuwa tayari tena kuwazuia[2] [3]. Wakati ule, Wajerumani wengi hawakuamini bado kwamba nchi itaunganishwa tena.[4]
Hatimaye mpaka ulifunguliwa tarehe 9 Novemba 1989[5]. Utawala wa Wakomunisti uliporomoka haraka na katika kipindi cha miezi 11 iliyofuata[6], masharti ya muungano yalijadiliwa kati ya Ujerumani Mashariki na Magharibi, Ufaransa, Uingereza, Marekani na Umoja wa Kisovieti.
Mkataba wa Masuluhisho ya Mwisho kuhusu Ujerumani uliotiwa saini na nchi hizo mbili ndani ya Ujerumani na nchi za washindi wa Vita Kuu ulifungua njia kuelekea kuungana tena[7][8][9].
Tarehe 3 Oktoba 1990, saa 00:01 majimbo matano ya Brandenburg, Mecklenburg-Vorpommern, Saxony, Saxony-Anhalt, Thuringia na Berlin yalijiunga rasmi na Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani. Jamhuri ya Kidemokrasia ya Ujerumani ilikoma kuwepo wakati huu.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Doder, Dusko; Branson, Louise (1990). Gorbachev: Heretic in the Kremlin. London: Futura. uk. 212. ISBN 978-0708849408.
- ↑ Thomas Roser: DDR-Massenflucht: Ein Picknick hebt die Welt aus den Angeln (German - Mass exodus of the GDR: A picnic clears the world) in: Die Presse 16 August 2018.
- ↑ Miklós Németh in Interview with Peter Bognar, Grenzöffnung 1989: „Es gab keinen Protest aus Moskau" (German - Border opening in 1989: There was no protest from Moscow), in: Die Presse 18 August 2014.
- ↑ THE WORLD; Despite New Stirrings, Dream of 'One Germany' Fades by Serge Schmemann, The New York Times, 14 May 1989
- ↑ http://news.bbc.co.uk/onthisday/hi/witness/november/9/newsid_3241000/3241641.stm 1989: The night the Wall came down, tovuti ya BBC "On this day" 9th November
- ↑ "GHDI - Document".
- ↑ American Foreign Policy Current Documents 1990 (Septemba 1990). "Treaty on the Final Settlement with Respect to Germany" (PDF). Roy Rozenweig Center for History and New Media. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2018-12-02. Iliwekwa mnamo 2021-12-09.
{{cite web}}
:|last=
has generic name (help)CS1 maint: date auto-translated (link) CS1 maint: numeric names: authors list (link) - ↑ "Treaty on the Final Settlement with Respect to Germany". Foothill College.
- ↑ Hailbronner, Kay. "Legal Aspects of the Unification of the Two German States" (PDF). European Journal of International Law. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2017-08-29. Iliwekwa mnamo 2021-12-09.
Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]- The Unification Treaty (Berlin, 31 August 1990) website of CVCE (Centre of European Studies)
- Hessler, Uwe, "The End of East Germany", dw-world.de, 23 August 2005.
- Berg, Stefan, Steffen Winter and Andreas Wassermann, "Germany's Eastern Burden: The Price of a Failed Reunification", Der Spiegel, 5 September 2005.
- Wiegrefe, Klaus, "An Inside Look at the Reunification Negotiations"Der Spiegel, 29 September 2010.
- "Unfriendly, even dangerous"? Margaret Thatcher and German Unification, Academia.edu, 2016.
- Problems with Reunification from the Dean Peter Krogh Foreign Affairs Digital Archives