Gatifloksasini
Gatifloksasini (Gatifloxacin), inayouzwa chini ya jina la chapa Tequin miongoni mwa zingine, ni dawa ya kukinga inayotumika kutibu maambukizi ya bakteria ya utando wa nje wa mboni ya jicho na kope la ndani.[1] Dawa hii inatumika kama tone la jicho.[1]
Madhara yake ya kawaida ni pamoja na maumivu ya jicho, ladha isiyo ya kawaida, na kuongezeka kwa wekundu wa macho.[1] Madhara yake mengine yanaweza kujumuisha athari za mzio.[1] Dawa hii iko katika familia ya fluoroquinolone na hufanya kazi kwa kuzuia vimeng'enya vya bakteria DNA gyrase na topoisomerase IV.[1]
Gatifloksasini ilipewa hati miliki mwaka wa 1986 na kuidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya kimatibabu mwaka wa 1999.[2] Michanganyiko ya mdomo na sindano iliondolewa nchini Marekani mwaka wa 2006 kutokana na madhara ya sukari ya juu au ya chini katika damu.[3]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 "Gatifloxacin (EENT) Monograph for Professionals". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 25 Novemba 2020. Iliwekwa mnamo 3 Desemba 2021.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Fischer, Jnos; Ganellin, C. Robin (2006). Analogue-based Drug Discovery (kwa Kiingereza). John Wiley & Sons. uk. 501. ISBN 9783527607495. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-10-31. Iliwekwa mnamo 2021-04-01.
- ↑ "Determination That TEQUIN (Gatifloxacin) Was Withdrawn From Sale for Reasons of Safety or Effectiveness". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 10 Mei 2021. Iliwekwa mnamo 3 Desemba 2021.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Gatifloksasini kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |