Gör Mahia
| ||
Gör Mahia ni klabu ya kandanda yenye makao yake katika mji mkuu wa Nairobi nchini Kenya. Ni kimojawapo kati ya vilabu viwili maarufu zaidi nchini katika kandanda ya vilabu nchini Kenya (klabu nyingine maarufu na mpinzani wake wa jadi ni AFC Leopards).
Gör Mahia imeshinda Ligi ya Kenya mara 21 na Kombe la Kenya mara nane. Gör Mahia ndiyo klabu ya kipekee nchini Kenya kushinda Taji la bara Afrika, kwani klabu hii ilishinda Kombe la Afrika la mabingwa mwaka wa 1987. Klabu hii ilianzishwa mwaka wa 1968 wakati vilabu viwili vya kandanda,Luo United na Luo Sports Club (pia ilikuwa inajulikana kama Luo Stars) , viliungana. Mmoja wa mwanzilishi wake alikuwa mwanasiasa Tom Mboya. Uwanja wao wa kucheza mechi za nyumbani ni Nairobi City Stadium.
Gör Mahia imeshinda shindano moja tu tangu mwaka wa 1995. Aidha, imeepuka kuteremshwa kwa ligi ya divisheni ya pili mara tatu. Licha ya matatizo yake ya kifedha, klabu hii ilikuwa inacheza vyema katika ligi msimu wa 2005-2006 lakini hatimaye mabishano mapya yaliharibu kila kitu.
Gör Mahia kama klabu inamizizi ya hekaya, hadithi na simulizi za Kiluo. Gör Mahia alikuwa shujaa wa Kiluo ambaye alikuwa anajulikana kwa umiliki wake wa mamlaka ambayo yalimwezesha kufanya maajabu. Mahia ni neno la Kiluo ambalo linaelezea ajabu na siri na hivyo basi wakati Gör ilianzishwa ilitakiwa kumiliki sifa asili za Gor Mahia kutokana na jina lake. Hakika Gör iliweza kudhibiti jina hilo na hata kupitisha matumaini ambayo watu wengi walitarajia. Katika miaka yake ya mafanikio, hakuna timu iliyoweza kupambana za Gör na baadhi ya watu waliona klabu hii kuwa bora barani Afrika. Sambamba na uaminifu wa wafuasi wake, Gör bado ina uwezo wa kusimama kutoka kwenye majivu na kurejea utukufuni walioupoteza kama "Gör wenye nguvu".
Klabu hii ilirejesha sifa yake ya kupata mataji mwaka wa 2008 wakati ilishinda Kombe la KFF. Hata hivyo, klabu zingine zote za KPL ziligoma kushiriki katika kombe hilo.
Historia
[hariri | hariri chanzo]Klabu hiyo ilianzishwa rasmi mnamo tarehe 17 Februari 1968 kama muungano wa Luo Union na Luo Sports Club (pia inajulikana kama Luo Stars ) na ikashinda ligi ya kitaifa kwa mara ya kwanza ya jaribio la ligi. Baadhi ya viongozi wake wa awali walikuwa wanasiasa Tom Mboya na Jaramogi Oginga Odinga . Walakini, klabu ilianzishwa mapema zaidi, mnamo 1915, na ilishiriki bila mpangilio wa mara kwa mara katika mashindano ya kiundani Magharibi mwa Kenya . Vikundi mbalimbali vilitumia jina hili kwa nyakati tofauti.
Klabu hiyo inacheza mechi zake za nyumbani katika uwanja wa Nairobi City Stadium . Vinginevyo, wanacheza pia katika uwanja wa Michezo wa Kimataifa wa Moi na Uwanja wa Kitaifa wa Nyayo . Awali imeandaa baadhi ya mechi katika Uwanja wa Kaunti ya Kisumu na Uwanja wa Manispaa ya Mombasa . [1]
Klabu hiyo ilishinda Ligi ya Kitaifa ya Soka ya Kenya mnamo 1968, baada ya kuanzishwa rasmi mnamo Februari mwaka huo huo. [2] Mnamo 1976, Gor Mahia ilishinda ligi ya kitaifa bila ya kupoteza mechi yoyote ya ligi, [3] [4] na kurudia rekodi yiyo hiyo miaka 39 baadaye chini ya usimamizi wa Frank Nuttall . [5]
Kuelekea mwishoni mwa miaka ya 2000, Gor ilianza kujizolea umaarufu kwa taratibu na kuwarudisha mashabiki wa soka wa Kenya uwanjani na kujaza mara kwa mara viwanja ambavyo tiketi zimekisha uzwa kwa ajili ya mechi hizo. Klabu ilirejea kwa medali ya fedha mwaka wa 2008 iliposhinda Kombe la KFF baada ya ukame wa miaka kumi na mitatu wa mataji yoyote makuu. Gor waliendelea kushinda Kenya DSTV Super Cup dhidi ya mabingwa watetezi wa mwaka huo, Mathare United kabla ya kuanza kwa msimu wa 2009 KPL . [6] Mnamo tarehe 26 Oktoba 2011 Gor Mahia kwa mtindo wa kutawala kwa kawaida iliwacharaza Sofapaka ndiposa kushinda toleo la 2011 la Kombe la FKL baada ya kuwashinda mahasimu wao wa jadi AFC Leopards siku 6 mapema katika tamasha la kusisimua la Siku ya Mashujaa la Oktoba 20. [7] [8]
Mataji
[hariri | hariri chanzo]- African Cup Winners 'Cup
- 1 (1987)
- Kombe la klabu za CECAFA
- 3 (1980,1981,1985)
- Ligi kuu ya Kenya
- 21 (1968, 1974, 1976, 1979, 1983, 1984, 1985, 1987, 1990, 1991, 1993, 1995, 2013, 2014, 2015, 2017, 2018, 2019, 2020, 2023, 2024)
- Kombe la KFF Cup
- 8 (1976, 1981, 1983, 1986, 1987, 1988, 1992, 2008)
- Kenya Super Cup
- 1 (2009)[9]
Utendaji katika mashindano ya CAF.
[hariri | hariri chanzo]- Kombe la shirikisho la CAF : tokeo 1
-
- 2008 - Raundi ya mchujo
- Kombe la Mabingwa wa klabu la Afrika : Matokeo 8
|
|
|
- Kombe la CAF : Matokeo 2
- 1974: Robo fainali
- 1971: Raundi ya kwanza
- Kombe la CAF la washindi:7
|
|
|
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Kisumu stadium renovation". Standard Digital News. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 29 Julai 2023. Iliwekwa mnamo 10 Septemba 2016.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "www.gorfc.com [13]". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 4 Machi 2016. Iliwekwa mnamo 10 Septemba 2016.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "When Gor Mahia won the league unbeaten". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 4 Machi 2016. Iliwekwa mnamo 10 Septemba 2016.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "It's derby time". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 17 Agosti 2016. Iliwekwa mnamo 10 Septemba 2016.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Willis, Seth (1 Novemba 2015). "Gor Mahia 2–0 Muhoroni Youth: Unbeaten K'Ogalo". Goal.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 4 Novemba 2015. Iliwekwa mnamo 1 Novemba 2015.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Gor Mahia Outclass Mathare United in Kenya Super Cup - Goal.com". 24 Januari 2009. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 11 Oktoba 2016. Iliwekwa mnamo 10 Septemba 2016.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Gor Mahia clinch FKL Cup". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 3 Machi 2016. Iliwekwa mnamo 10 Septemba 2016.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Untitled 1". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 30 Machi 2016. Iliwekwa mnamo 10 Septemba 2016.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ tovuti ya Daily Nation tovuti, 24 Januari 2009 Gor tear Mathare United apart
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Tovuti Rasmi
- Tovuti isiyo rasmi Ilihifadhiwa 8 Julai 2008 kwenye Wayback Machine.