Nenda kwa yaliyomo

Funke Opeke

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Funke Opeke


Funke Opeke
Nchi Nigeria
Kazi yake Mhandisi wa umeme


Funke Opeke ni mhandisi wa umeme kutoka Nigeria, mwanzilishi wa Main Street Technologies na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Main One Cable, kampuni ya huduma za mawasiliano iliyoko katika Jimbo la Lagos, kusini-magharibi mwa Nigeria[1],Kampuni yake iitwayo MainOne ni kampuni bora inayotoa huduma za mawasiliano na suluhisho la mtandao katika Afrika Magharibi [2]

Elimu na Maisha ya awali

[hariri | hariri chanzo]

Funke Opeke alisoma katika Shule ya Queens school (wasichana pekee) huko Ibadan katika jimbo la Oyo, Nigeria.[3] Alilelewa huko Ibadan katika mji mkuu wa Jimbo la Oyo,ingawa, yeye ni mzaliwa wa Ile- Oluji, jimbo la Ondo.Alizaliwa katika familia ya watoto 9, baba yake alikuwa mkurugenzi wa kwanza wa Taasisi ya Utafiti ya kokoa ya Nigeria wakati mama yake alikuwa mwalimu.[3]

Funke Opeke alipata shahada ya kwanza na shahada ya uzamili ya uhandisi wa umeme kutoka Chuo Kikuu cha Obafemi Awolowo na Chuo Kikuu cha Columbia,[4]Baada ya kuhitimu katika Chuo Kikuu cha Columbia, alifuata taaluma ya tehama nchini Marekani kama mkurugenzi mtendaji katika kitengo cha jumla cha Mawasiliano cha Verizon huko New York City. Mnamo 2005, alijiunga na MTN Nigeria kama afisa mkuu wa ufundi.[5][6]

  1. AfICTA. "Profile: Funke Opeke". AfICTA (kwa Kiingereza (Uingereza)). Iliwekwa mnamo 2022-03-16.
  2. "Africa's Leading Women - Funke Opeke |". web.archive.org. 2019-03-23. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-03-23. Iliwekwa mnamo 2022-03-16.
  3. 3.0 3.1 Titilola Oludimu (2017-05-05). "5 things you didn't know about Funke Opeke, CEO of MainOne". Techpoint Africa (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2022-03-16.
  4. "Bloomberg - Are you a robot?". www.bloomberg.com. Iliwekwa mnamo 2022-03-16. {{cite web}}: Cite uses generic title (help)
  5. "Shittu, Ndukwe, Ovia, others to enter DS-IHUB hall of fame". Vanguard News (kwa American English). 2016-07-13. Iliwekwa mnamo 2022-03-16.
  6. admin (2016-08-11). "Govt Urged to Leverage Power of Broadband Technology". THISDAYLIVE (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2022-03-16.