Nenda kwa yaliyomo

Foolish Age

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Follish age)

Foolish Age ni filamu ya Kitanzania iliyotolewa mwaka 2013. Iliandaliwa na Elizabeth Michael.[1]

Filamu hii inachanganua ushawishi hasi wanaokutana nao vijana walio katika balehe.

Filamu hii inaelezea hadithi ya Loveness (Elizabeth Michael) msichana mdogo aliyelelewa na baba tajiri baada ya kifo cha mama yake kwa Ugonjwa wa UKIMWI miaka kadhaa iliyopita. Loveness na baba yake pia wanaishi na virusi vya UKIMWI. Loveness anasoma ughaibuni ila baadaye anamlazimisha baba yake aje kusoma Nchini mwake, Tanzania. Anapata shule mpya na kutengeneza marafiki, lakini rafiki wake wa dhati (Diana Kimaro) siyo msichana mwema. Wanajihusisha na mapenzi katika umri mdogo na wanaume tofauti tofauti. Wanaacha kwenda shule kwa sababu ya maisha ya klabu na kubadili wanaume. Loveness anaondoka katika nyumba nzuri ya baba yake pasipo kumuaga baba yake na kwenda kuishi maisha ya ghetto. Baba yake anamtafuta kila mahali pasipo mafanikio mwishowe anakata tamaa. Loveness anaendelea na maisha ya aina hiyo lakini baadaye anakumbana na ugumu wa wa maisha, manyanyaso ya kingono na matatizo na marafiki zake.

Washiriki

[hariri | hariri chanzo]
  • Elizabeth Michael
  • Diana Kimaro
  • Hashim Kambi
  • Emmylia Joseph
  • Ombeni Phiri
  • Mandela Nicholaus
  • Ramadhani Miraji
  • Mohamed Fungafunga (billed on the poster under alias "Jengua")[2]
  • Zamaradi Salim
  • Soud Ali
  • Idrisa Makupa
  • Leah Mussa
  • Tiko Hassan[3]
  1. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2024-02-22. Iliwekwa mnamo 2020-10-10.
  2. "Mohammed Fungafunga | Actor, comedian, — Bongo Movies - Buy Tanzania Movies and DVD's Online". www.bongocinema.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-01-15. Iliwekwa mnamo 2018-01-14. {{cite web}}: More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help)
  3. "Foolish Age — Bongo Movie | Tanzania". www.bongocinema.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2024-02-22. Iliwekwa mnamo 2018-01-14. {{cite web}}: More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help)
Makala hii kuhusu filamu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Foolish Age kama waigizaji wake, hadithi au matoleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.