Fludroxycortide
Jina la Utaratibu la (IUPAC) | |
---|---|
6-Fluoro-11,21-dihydroxy-16,17-[(l-methylethylidene)bis(oxy)]-(6α,11β,16α)-pregn-4-ene-3,20-dione | |
Data ya kikliniki | |
Majina ya kibiashara | Cordran, Haelan, mengineyo |
AHFS/Drugs.com | Monograph |
Kategoria ya ujauzito | ? |
Hali ya kisheria | POM (UK) |
Njia mbalimbali za matumizi | Juu ya ngozi |
Vitambulisho | |
Nambari ya ATC | ? |
Visawe | Flurandrenolide, flurandrenolone |
Data ya kikemikali | |
Fomyula | C24H33FO6 |
| |
(hii ni nini?) (thibitisha) |
Fludroxycortide, pia inajulikana kama flurandrenolide na flurandrenolone, ni dawa ya steroidi ya kupaka kwenye ngozi inayotumika kutibu magonjwa ya ngozi kama vile eczema na psoriasis.[1] [2] Dawa hii inatumika kwa ngozi mara moja hadi mbili kwa siku.[2]
Madhara yake yanaweza kujumuisha hatari ya kuambukizwa, athari za mzio, chunusi, kudhoofika kwa ngozi na michirizi ya ngozi (striae).[2][1] Ni mara chache sana ugonjwa wa Cushing unaweza kutokea.[1] Matumizi yake ya muda mrefu au ya kina hayapendekezwi wakati wa ujauzito.[3] Dawa hii ni ya nguvu ya kati hadi ya juu.[2][1]
Fludroxycortide iliidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya kimatibabu nchini Marekani mwaka wa 1965[1] na inapatikana kama dawa ya kawaida.[2] Nchini Uingereza, gramu 60 iligharimu takriban £6 kufikia mwaka wa 2021.[2] Nchini Marekani, kiasi hiki kinagharimu dola 46.[4]
Marejeleo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 "Flurandrenolide Monograph for Professionals". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 3 Machi 2016. Iliwekwa mnamo 14 Desemba 2021.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 2.0 2.1 2.2 2.3 2.4 2.5 BNF 81: March-September 2021. BMJ Group and the Pharmaceutical Press. 2021. uk. 1290. ISBN 978-0857114105.
- ↑ "Flurandrenolide topical Use During Pregnancy". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2 Desemba 2020. Iliwekwa mnamo 14 Desemba 2021.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Flurandrenolide Prices, Coupons & Savings Tips - GoodRx". GoodRx. Iliwekwa mnamo 14 Desemba 2021.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)