Nenda kwa yaliyomo

Florence Ievers

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Florence Ievers ni wakili wa Kanada, ambaye amefanya kazi kama mtumishi wa umma. Kati ya mwaka 1997 na 2007 aliteuliwa na kuthibitishwa kama Msimamizi wa Wanawake wa Kanada kila mwaka. Nafasi hiyo sio uteuzi wa kisiasa lakini inahitaji uteuzi kutoka kwa waziri.[1][2] Mwaka 2002, alichaguliwa kuwa Makamu wa Raisi wa Tume ya Kimataifa ya Wanawake wa Amerika na alitumikia kuanzia mwaka 2003 hadi 2005.[3]

Kati ya tarehe 11 na 15 Julai 2002, Ievers na wengine walihudhuria Mkutano wa Kimataifa wa Wanawake uliofanyika Barcelona, Uhispania, kama sehemu ya ujumbe wa kutathmini jinsi serikali zinaweza kuelekeza vyema misaada kwa miradi ya biashara za wanawake.[4] Alikuwa mgombea wa Liberal katika uchaguzi wa mwaka 1984 kwenye nafasi ya Mbunge wa Langelier, Quebec, akishindwa na Michel Coté.[5] Kati ya mwaka 1982 na 1984, Ievers alifanya kazi katika ofisi ya Waziri Mkuu Pierre Trudeau na kama katibu wa uteuzi na baadaye alisimamia mpango wa serikali kwa wanawake.[6] Awali, aligombea katika uchaguzi wa mwaka 1981 kwa Wilaya ya Taschereau na pia akashindwa.[7]

  1. Turcotte, Jeremy (20 Aprili 2015). "Better know a Canadian functionary: the Coordinator of Status of Women Canada". Canada: Jeremy Turcotte. Iliwekwa mnamo 11 Septemba 2015.
  2. "38th PARLIAMENT, 1st SESSION Standing Committee on the Status of Women". House Publications. Ottawa, Ontario, Canada: Parliament of Canada. 21 Juni 2005. Iliwekwa mnamo 11 Septemba 2015.
  3. "31st Assembly of Delegates (Punta Cana, Dominican Republic, October 29-31, 2002)". Organization of American States. Washington, DC: Inter-American Commission of Women. Iliwekwa mnamo 11 Septemba 2015.
  4. Robertson, Krista (16 Septemba 2002). "Global Summit of Women" (PDF). CanadExport. 20 (15). Canada: Idara ya Mambo ya Nje na Biashara ya Kimataifa: 14. Iliwekwa mnamo 11 Septemba 2015.
  5. "LANGELIER, Quebec (1968 - 1990)". Ottawa, Ontario, Canada: Parliament of Canada. Iliwekwa mnamo 11 Septemba 2015.
  6. "Fonds the Rt. Hon. Pierre Elliott Trudeau: Staff Series 1968-1984" (PDF). Archives of Canada. Canada: Political Archives Section, Manuscript Division. Iliwekwa mnamo 11 Septemba 2015.
  7. "Élection générale: 13 avril 1981 (carte électorale de 1980)" (kwa Kifaransa). Québec, Canada: Québec Politique. Iliwekwa mnamo 11 Septemba 2015.
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Florence Ievers kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.