Nenda kwa yaliyomo

Flora M’mbugu-Schelling

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Flora M’mbugu-Schelling ni mtayarishaji wa makala nchini Tanzania, anayejulikana zaidi kupitia makala iitwayo "These Hands" (Mikono Hii).

Flora M’mbugu-Schelling alipata elimu yake katika Chuo cha Uandishi wa [habari]] Tanzania (Tanzania School of Journalism) kabla ya kwenda kujiendeleza kielimu nchini Ujerumani na Ufaransa.

Kazi yake ya kwanza kumtambulisha kwenye tasnia ya filamu ilijulikana kama "Kumekucha" (1987) na kushinda medali ya dhahabu katika tamasha la kimataifa la filamu la Newyork. Makala yake ya "These Hands" ilihusu wanawake wa Msumbiji waliokuwa wakifanya kazi ya kuvunja kokoto katika machimbo nchini Tanzania.

  • Kumekucha,1987
  • These Hands (Mikono Hii),1992
  • Shida na Matatizo,1993
  1. Bisschoff, L. (2014) Women's stories and struggles in "These Hands" (Flora M'mbugu-Schelling). In: Bisschoff, L. and Murphy, D. (eds.) Africa's Lost Classics: New Histories of African Cinema. Legenda: Oxford. ISBN 9781907975516
  2. Claire Robertson,Film Reviews,The American Historical Review, Vol. 101, Issue 4, October 1996, pp.1142-3.
  3. Flora M’mbugu-Schelling, African Film Festival.
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Flora M’mbugu-Schelling kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.